Sunday , 12 May 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Dk. Mpango awatumia ujumbe viongozi wanaojilimbikizia mali
Habari za Siasa

Dk. Mpango awatumia ujumbe viongozi wanaojilimbikizia mali

Spread the love

MAKAMU wa Rais, Dk. Phillip Mpango, amewataka viongozi wa umma wanaotumia nyadhiofa zao kujilimbikizia mali, wajitafakari. Anaripoti Mwandishi Wetu, Manyara…(endelea).

Dk. Mpango ametoa agizo hilo leo tarehe 14 Oktoba 2023 katika kumbukizi ya miaka 24 ya kifo cha Baba wa Taifa, Hayati Mwalimu Julius Nyerere, iliyofanyika mkoani Manyara.

“Baba wa taifa alichukia sana rushwa, hakuvumilia vitendo vyovyote vyenye harufu ya rushwa wala ufisadi. Ni wajibu wetu kuyaishi haya.

Alithamini sana thamani ya dhamana aliyopewa hakutumia cheo chake kwa faida yake, hata nyumba yake ya Butiama alijenegwa na Serikali sasa viongozi tujitafakari wale wanaojilimbikizia mali na kutumia vibaya nafasi zao sio njia njema ya kumuenzi,” amesema Dk. Mpango.

Katika hatua nyingine, Dk. Muhongo amewataka watanzania kumuenzi Mwalimu Nyerere kwa kupinga rushwa na fitina, huku akiwataka viongozi wa umma kufuata nyayo zake za kuomba radhi kwa wananchi pale anapokosea.

“Elimu yake na vipaji alivyopewa kwa faida ya wote alivitumia kupiga vita umasikini. Wote tunafahamu ni kweli alikuwa mwalimu hodari kufundisha, lakini alikuwa mkweli hakutaka fitina na sisi tujitahidi kukwepa kuwa wafitini.,” amesema Dk. Mpango na kuongeza:

“Alikuwa mnyenyekevu hakusita kujisahihisha alipotambua kakosea na sisi viongozi kwa wananchi pale ambapo tunakosea tukiri tunakosea na tujisahihishe.”

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Dk. Biteko: Serikali itaendelea kushirikiana na Red Cross

Spread the loveNaibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Doto Biteko...

Habari MchanganyikoHabari za SiasaTangulizi

Dk.Mpango aagiza trafki kuvaa makoti ya kamera kudhibiti rushwa

Spread the loveMakamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk....

Habari za SiasaKimataifa

Palestina mwanachama wa 194 wa UN

Spread the loveBaraza Kuu la Umoja wa Mataifa jana Ijumaa limepitisha kwa...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Vijana UVCCM Kagera wataka mwenyekiti wao ajiuzulu

Spread the loveVIJANA wa Chama cha Mapinduzi Mkoa wa Kagera wamemtaka Mwenyekiti...

error: Content is protected !!