Sunday , 28 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Samia ataka ripoti miradi ya bilioni 1.9 yenye dosari
Habari za SiasaTangulizi

Samia ataka ripoti miradi ya bilioni 1.9 yenye dosari

Spread the love

RAIS Dk. Samia Suluhu Hassan, ameagiza apewe ripoti ya hatua zilizochukuliwa dhidi ya watumishi wa umma waliohusika katika usimamizi wa miradi saba yenye thamani ya Sh. 1.9 bilioni, ambayo mbio za mwenge zimebainisha kuwa ina dosari. Anaripoti Mwandishi Wetu, Manyara…(endelea).

Rais Samia ametoa agizo hilo leo tarehe 14 Oktoba 2023, akishriki kilele cha mbio za mwenge, mkoani Manyara.

“Wakati wa mbio za mwenge kuna miradi mbalimbali imebainika kuwa na dosari katika utekelezaji wake, ikiwemo ubadhirifu, ucheleweshaji, kuwa chini ya viwango vya ubora. Miradi 1,424 yenye thamani ya Sh. 5.3 trilioni, ilishughulikia katika halmashauri 195, kati ya hiyo saba ndiyo iliyobainika kuwa na dosari,” amesema Rais Samia.

Rais Samia amesema “niwaonye wale ambao bado wanaichukulia kazi yao waliyopelekwa kutumikia wananchi ni ya kawaida, waende wakajirekebishe. Nataka mamlaka zinazohusika ziwe zinawasilisha katika ofisi ya waziri mkuu taarifa kuhusu hatua zilizochukuliwa na inifikie mimi kabla ya maadhimisho yanayofuata ya mwenge.”

Katika hatua nyingine, Rais Samia amewataka wananchi waimarishe umoja, uwajibikaji pamoja na kufanya kazi kwa bidii na kujitegemea, ili kulinda uhuru wa Tanzania.

Rais Samia amesema Serikali yake inaendelea kutekeleza mipango ya kuwawezesha vijana washiriki katika shughuli za kiuchumi ili wasiwe mizigo kwa taifa, ikiwemo kujenga vyuo vya ufundi ambapo kwa sasa vyuo 64 vinaendelea kujengwa wakati vingine 50 vikiwa mbioni.

“Na sasa tumedhamiria kujenga taifa linalojitegemea, kwa mujibu wa sense ya watu na makazi ya mwaka jana vijana ni asilimia kubwa na ndiyo tegemeo kuu la nguvu kazi ya ujenzi wa taifa letu. Sasa nguvu kazi hii ikikosa muelekeo na kushindwa kujituma ipasavyo inaweza kuwa mzigo kwa taifa,” amesema Rais Samia.

Akizungumzia kauli mbiu ya kilele cha mbio za mwenge inayohimiza utunzaji wa mazingira, Rais Samia ameagiza kampeni za upandaji miti ziendelee pamoja na tunzaji wa vyanzo vya maji ili kukwepa mabadiliko ya tabia ya nchi.

Rais Samia amewataka wananchi waepukane na tabia ya kuchoma moto mashamba kiholela, kwa kuwa vitendo hivyo vinaathiri mazingira.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Biteko aipongeza GGML kudhibiti vifo, majeruhi mahali pa kazi

Spread the loveNAIBU Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Doto Biteko...

Habari za Siasa

Askofu Shoo awataka ACT kupigania maslahi ya Taifa, wasikubali kuhongwa

Spread the loveALIYEKUWA Askofu Mkuu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri, Askofu...

Habari za Siasa

Biteko aagiza waajiri kudhibiti vifo mahali pa kazi

Spread the love  NAIBU Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Doto...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Mavunde aibana kampuni kutimiza masharti ya mkataba

Spread the loveWaziri wa Madini, Anthony Mavunde ameitaka Kampuni ya Xin Tai...

error: Content is protected !!