Monday , 13 May 2024
Home Kitengo Biashara Rais Samia aikabidhi tuzo maalum Benki ya NMB
Biashara

Rais Samia aikabidhi tuzo maalum Benki ya NMB

Spread the love

RAIS wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan ametoa tuzo maalum kwa benki ya NMB katika kutambua mchango na utendaji mkubwa wa taasisi hiyo ya fedha nchini. Anaripoti Mwandishi Wetu…(endelea).

Tuzo hizo alizitoa jana Jumamosi, Agosti 19, 2023 katika kikao kazi cha watendaji wakuu wa taasisi na masharika ya umma pamoja na wenyeviti wao wa bodi, kinachofanyikia jijini Arusha na kitahitimishwa kesho Jumatatu, Agosti 21, 2023.

 

Rais Samia Suluhu Hassan akimkabidhi   Afisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya NMB, Ruth Zaipuna pamoja na Mwenyekiti wabodi ya NMB, Dk. Edwin Mhede, cheti cha mlipa gawio kubwa serikalini wakati wa  kikao kazi cha wenyekiti wa bodi na watendaji wakuu  wa taasisi za umma jijini Arusha. Benki hiyo ambayo serikali ina mmiliki asilimia 31.8 ilitoa gawio la biliioni 45.5  mwaka fedha 2021- 2022.

Rais Samia alisema pamoja na kuwapongeza wale waliofanya vizuri, Serikali pia itafanya tathmini ya utendaji wa taasisi na mashirika mengine ya Tanzania.

“Kupitia mashirika Serikali inaweza kukusanya fedha nyingi za kutosha kujazia upungufu wa bajeti ya nchi na hivyo kuipunguzia serikali mzigo wa kwenda kukopa nje,” alisema Rais Samia.

Rais Samia alisisitiza taasisi zingine ziige mfano wa zile zinachangia kasma ya Taifa kupitia gawiwo serikalini.

“Ni muhimu sana ofisi ya msajili wa hazina ihakikishe inasimamia ipasavyo sheria na Kanuni zilizopo katika kuhakikisha kuwa taasisi za umma zinajiendesha kwa tija na kuipunguzia serikali mzigo wa gharama za kuziendesha,” alisema Rais Samia.

Benki ya NMB imetoa gawio la shilingi Billioni 45.5 serikalini katika mwaka wa fedha uliopita wa 2022/23.

Pamoja na kutoa pongezi kwa Benki ya NMB, Rais Samia pia alimkabidhi cheti cha mlipa gawiwo kubwa serikalini setka ya kibenki, Afisa Mtendaji Mkuu wa taasisi hiyo, Ruth Zaipuna.

Kwa mujibu wa Msajili wa Hazina, Nehemiah Mchechu, Serikali inamiliki asilimia 31.8 ya hisa katika benki ya NMB.

“Tumetoa tuzo kwa taasisi zilizofanya vizuri ili kuleta changamoto katika kujifunza sisi sote na ili taasisi zingine ziwe na wivu wa kusonga mbele ndio tuweze kuisaidia nchi yetu,” alisema Mchechu.

Kwa mujibu wa Msajili huyo wa Hazina, Serikali imewekeza zaidi ya shilingi Trillioni 73 katika taasisi za umma na kwamba ni jukumu lao kuhakikisha fedha hizo zinazaa matunda makubwa katika kukuza uchumi wa nchi.

“Tunatarajia kuwa siku za mbeleni pamoja na kuwa na list of fame (orodha ya sifa), ya taasisi zinazofanya vizuri, baadae pia tungeweza kuwa na list of shame (ordha ya aibu) kwa taasisi zinazofanya vibaya lakini hatutarajii kufika huko, kutokana na maboresho makubwa tunayofanya kwa taasisi hizi kwa sasa,” alisema Mchechu.

Jumla ya taasisi 248 zimeshiriki mkutano huo wa kwanza wa mwaka wa kikao Kazi cha wenyekiti wa bodi na watendaji wakuu wa taasisi za umma ukiwa na washiriki zaidi ya 600.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Biashara

Vuna mapene hadi Mil 400 ukicheza Expanse Tournament 

Spread the love  Promosheni ya kuvuna mahela ya Meridianbet bado inaendelea kusaka...

Biashara

Cheza Meridianbet kasino shinda mamilioni na Hot Shots

Spread the love  Hii ni kwa wapenzi wa michezo isiyo ya kasino...

Biashara

Meridianbet yatoa msaada Kigamboni siku ya Mama Duniani

Spread the loveMABIBGWA wa michezo ya kubashiri kampuni yaMeridianbet imefika kigamboni leo siku...

BiasharaHabari Mchanganyiko

PPAA yajipanga kuwanoa wazabuni namna kuwasilisha rufaa kieletroniki

Spread the loveIli kukabiliana na mageuzi yaliyofanyika katika Sheria mpya ya Ununuzi...

error: Content is protected !!