Sunday , 28 April 2024
Home Kitengo Biashara Ya Rwanda yanatufunza tusiingize dini kwenye siasa
Biashara

Ya Rwanda yanatufunza tusiingize dini kwenye siasa

Spread the love

Tumsifu Yesu Kristo, Amani na Usalama. Nataka niwape tafakari ndogo ya sehemu ya Kanisa Katoliki katika amani na ustawi wa jamii yetu.

Naomba nitumie mfano wa jirani zetu Rwanda mwaka 1994. Idadi ya Wakatoliki ilikuwa 65%, Waprotestanti 9%, Waislamu 1%. Dini nyingine na wasio na dini wanagawana hiyo 25% inayobaki.

Kama tunavyojua Rwanda ina makabila makubwa mawili, Wahutu na Watusi. Maaskofu akiwemo aliyekuwa Askofu Mkuu wa Kigali Vincent Nsengiyumva, wakawa nyuma ya siasa za kibaguzi kwa miaka 14.

George Rugambwa

Askofu Nsengiyumva akawa Mwenyekiti wa Kamati Kuu ya National Republican Movement for Democracy and Development (NRMDD) au Kiswahili Vuguvugu la Jamhuri la Demokrasia na Maendeleo. Hiki kilikuwa ndicho chama tawala chini ya Wahutu kuanzia mwaka 1975 hadi mwaka 1994 pale Kagame na Rwandan Patriotic Front (RPF) walipoitwaa Kigali baada ya watu zaidi ya 800,000 wengi wao Watusi kupoteza maisha katika mauaji ya Kimbari.

Mwaka 1990 Vatican ilimuonya Askofu Nsengiyumva kuachana na siasa lakini hakutii ipasavyo. Sijui kama mnaelewa. Huyu alikuwa Askofu Mkuu wa Kanisa Katoliki Kigali Rwanda na wakati huo huo Mwenyekiti wa Kamati Kuu ya Chama Tawala na Kiongozi wa Maaskofu wote wa Katoliki Rwanda.

Chama chake cha Wahutu kilishiriki kupanga mauaji ya Watusi. Chini ya uongozi wake maaskofu Rwanda waliishi kwenye majumba ya kifahari yakijengwa kwa misamaha ya kodi kwenye huduma na biashara za kanisa.

Juni 7 1994, kikosi kidogo cha Wanajeshi wa Kagame wa RPF walimvamia na kumuua yeye na maaskofu wengine wawili na mapadri kumi na kusema wanahusika kwenye mauaji ya ndugu zao.

Askofu Nsengiyumva alikuwa na marafiki maaskofu, mapadri na watawa Tanzania na amefika hapa mara nyingi hadi miaka miwili kabla ya kifo chake.

Wakristo wenzangu, nachotaka kusema ni kwamba viongozi wetu wa dini ni binadamu wenye ajenda zao. Uzuri baadhi ya mambo yao mnayajua pia. Akili za kuambiwa changanya na za kwako.

Nawatakia Ibada Njema ya Jumapili Agosti 20 2023.  Mwandishi wa makala haya ni George Rugambwa kutoka Butainamwa, Kagera.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Biashara

Maisha ya kasino ni furaha, cheza Book of Eskimo kujichukulia utajiri 

Spread the love  KUPNGA ni kuchagua, chagua kuwa mshindi kila siku kupitia...

Biashara

Sloti ya Mega Jade kasino njia 10 za malipo unaposhinda

Spread the love  TUNAKULETEA mchezo wa kasino wa kufurahisha sana ambapo unapewa...

Biashara

Orb of Destiny kutoka Meridianbet kasino ushindi kwa njia 14  

Spread the love  ORB of Destiny ni mchezo wa sloti kutoka kwa...

Biashara

Jiandalie Strawberry Cocktail yako nyumbani huku unacheza kasino 

Spread the love  UTAANDAA matunda yako unayotaka kutumia unaweza kutumia Strawberry, Cantaloupe...

error: Content is protected !!