Saturday , 27 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Kikwete: Tuwanyanyapae wanaochanganya dini, siasa
Habari za SiasaTangulizi

Kikwete: Tuwanyanyapae wanaochanganya dini, siasa

Spread the love

RAIS Mstaafu Jakaya Kikwete amewataka Watanzania kuwanyanyapaa viongozi wanaochanganya dini na siasa kwa kuwa ni jambo hatari kwa ustawi wa amani na utulivu wa Taifa. Anaripoti Mwandishi Wetu …(endelea).

Kikwete ametoa kauli hiyo leo tarehe 20 Agosti 2023 wakati akizungumza katika ufunguzi wa jengo Kanisa la Kiadventisti Wasabato Mara.

Kikwete amesema siku ikifika ambapo uanachama wa chama cha siasa au uumini thabiti wa dini ukawianishwa na chama cha siasa anachokifuata kiongozi yeyote ndio mwisho wa Taifa.

Ameongeza kuwa hali ikiwa hivyo Tanzania itakuwa na vyama vya siasa vya wakristu, waislamu na walokole.

“Napenda pia kuwaonya, tusijaribu kuchanganya dini na siasa na kama kuna viongozi wanataka kutuelekeza kwa kutumia dini kwa manufaa ya siasa au kama kuna viongozi wa siasa wanataka kutumia dini kwa manufaa yao ya kisiasa naombeni ndugu zangu tuwanyanyapae.

“Pia watu kutazama masuala ya dini kwa mtazamo wa siasa za vyama vyao si jambo la afya kwa zetu. Yote mawili yataathiri umoja, usalama na kutishia amani na utulivu tunaoufaidi sasa,” amesema.

Kikwete ameenda mbali zaidi na kutoa mfano namna alivyohaha kutafuta suluhu Visiwani Zanzibar baada ya kuathiriwa na dini na siasa.

“Zanzibar walifika mahali wanamuona Shekh ambaye ni mfuasi wa chama ambacho sio chake sio Sheikh sawasawa. Kwa hiyo wakienda kusali kama Sheikh ni mfuasi wa CUF wanangoja amalize kusalisha alafu anaingia sheikh wa CCM na waislamu wake.

“Nawaambie vitu halisi ndio maana nilipokuwa rais nikashughulika sana pale kupata ule miafaka, niliahidi ile hotuba yangu ya kwanza ya Bunge 2005 Disemba 30 kwamba nitafanya kila ninaloliweza tujenhe muafaka Zanzibar,” amesema.

Amesema kazi hiyo haikuwa rahisi katika mkutano huo wa miafaka iliofanyia Butiama.

“Ilikuwa moja ya kikao kigumu kwelikweli lakini nikasema pamoja na ugumu wote lazima hapa tuvuke, tukafika mahali nilipoona mambo yamekuwa makali nilichojifunza duniani nikasema tuendeni kwanza tukale.

“Tulipoenda kula ndio tukaweka mikakati ya kumaliza hizi jambo. Tukajipanga nani ataanza kuzungumza nani atafuatia tukakubaliana kuwa na serikali ya umoja wa kitaifa,” amesema.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

ACT: Waongoza watalii wapate maslahi yao inavyostahili

Spread the loveCHAMA cha ACT-Wazalendo kimeitaka serikali kuhakikisha inasimamia maslahi stahiki ya...

Habari za SiasaTangulizi

Prof. Lipumba ajitosa kuviunganisha vyama vya siasa Burundi

Spread the love  MWENYEKITI wa Kituo Cha Demokrasia Tanzania (TCD), Prof. Ibrahim...

Habari za SiasaTangulizi

Samia awataka watanzania kudumisha muungano

Spread the loveRais wa Tanzania,Samia Suluhu Hassan amewataka Watanzania kuendeleza Muungano kwa...

Habari za Siasa

Prof. Muhongo akomalia matumizi nishati jadidifu kuondoa uhaba wa umeme

Spread the love  MBUNGE wa Musoma Vijijini (CCM), Profesa Sospeter Muhongo, ameendelea...

error: Content is protected !!