Thursday , 9 May 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Sakata la Dk. Slaa na wenzake: Polisi kuburuzwa kortini
Habari za SiasaTangulizi

Sakata la Dk. Slaa na wenzake: Polisi kuburuzwa kortini

IGP Camillius Wambura
Spread the love

MAWAKILI wa Dk. Willibord Slaa na wenzake watatu, wako mbioni kufungua shauri Mahakama Kuu, Kanda ya Mbeya, kuomba amri ya kuwataka jeshi la polisi, kuwafikisha mahakamani wateja wao. Anaripoti Mwanadishi Wetu…(endelea).

Dickson Matata, wakili wa Dk. Slaa, ameliambia MwanaHALISI kuwa yeye na mwenzake, Philip Mwakilima, wameamua kwenda mahakamani kufungua shauri dhidi ya polisi, baada ya kujiridhisha kuwa hakuna dalili za kuwafikisha watuhumiwa mahakamani.

“Tunakwenda mahakamani ili ‘ku-file’ (kufungua) ‘Habeas corpus!’ tunakwenda mahakamani baada ya kuona jeshi la polisi, linavunja sheria kwa kuendelea kubaki na watuhumiwa, kinyume na Katiba,” ameeleza.

Aliongeza: “Habeas corpus,’ ni dhana ya Kilatini ikitumika kisheria kuelezea kitendo cha mamlaka kumshikilia au hata kumfunga mtu kinyume cha sheria, ili Mahakama ilazamishe wahusika wafikishwe mahakamani.”

Dk. Slaa, pamoja na wenzake wawili – Boniface Mwabukusi, wakili wa Mahakama Kuu na mtetezi mkubwa wa rasimali za umma, pamoja na Mpaluka Nyagali (Mdude), mwanachama wa upinzani, wako mikononi mwa polisi, tangu wiki iliyopita.

Wanatuhumiwa kupanga na kuandaa maandamano ya nchi nzima, yanayodaiwa kulenga “kuipindua serikali.”

Tuhuma zinazowakabili zinaangukia kwenye mashitaka ya uhaini, ambayo kwa mujibu wa sheria za Tanzania halina dhamana.

Wanaotajwa na kujitambulisha kuwa watetezi wakuu wa rasimali za umma, wamekuwa wapinzani wakubwa wa mkataba wa uwekezaji kati ya serikali na kampuni ya DP World ya Falme za Kiarabu.

Naye Askofu Emmaus Mwamakula, ameendekea kulitolea wito jeshi la polisi kuacha kuvunja Katiba.

Amesema, “kama jeshi la polisi halina mashitaka liwaachie huru watuhumiwa kuliko kuendelea kuvunja katiba ya nchi na kuendelea kufinya haki za raia.”

Watuhumiwa hao watatu, wamekuwa mstari wa mbele kupinga mkataba wa uwekezaji kati ya kampuni ya kigeni ya DP World kutoka Dubai na Mamlaka ya Bandari (TPA).

Mwabukusi aliongoza jopo la wanasheria waliofungua kesi Mahakama Kuu, kupinga uwekezaji huo kwa madai kuwa ndani ya mkataba kumesheheni vifungu vinavyopingana na Katiba na unahatarisha uhuru na usalama wa taifa.

Makubaliano hayo yanaweka mfumo wa kisheria kwa Dubai kushirikiana na Tanzania katika maendeleo, usimamizi na uendeshaji wa bandari zilizoko kanda maalum za kiuchumi (SEZ), korido za biashara na bandari kavu (ICD), yalisainiwa Oktoba mwaka jana.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Serikali yapunguza kodi ya makampuni kwa 20%

Spread the loveSERIKALI imepunguza kodi ya makampuni kwa asilimia 20, kutoka asilimia...

Habari za SiasaTangulizi

Lissu, Halima Mdee hapatoshi

Spread the loveVITA ya maneno kati ya Makamu Mwenyekiti wa Chama cha...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Madiwani Msalala wampa tano DED kwa kuongeza mapato

Spread the loveMKURUGENZI wa Halmashauri ya Wilaya ya Msalala, mkoani Shinyanga, Khamis...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Kimbunga Hidaya chaua 5, kaya 7,027 zikikosa makazi

Spread the loveSERIKALI imetoa tathmini ya athari za kimbunga Hidaya, kilichotokea tarehe...

error: Content is protected !!