Saturday , 27 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Rais Samia awapangia vituo mabalozi 3, Kipilimba, Migiro warejeshwa
Habari za SiasaTangulizi

Rais Samia awapangia vituo mabalozi 3, Kipilimba, Migiro warejeshwa

Spread the love

RAIS Samia Suluhu Hassan amewapangia vituo vya kazi Mabalozi watatu na kumbadilishia kituo cha kazi Balozi mmoja. Anaripoti Mwandishi Wetu …(endelea).

Pia Balozi wa Tanzania nchini Uingereza, Dk. Asha Rose Migiro amerejeshwa baada ya kumaliza mkataba wake huku Balozi wa Tanzania nchini Namibia, Dk. Modestus Kipilimba akirejeshwa baada ya kustaafu.

Taarifa iliyotolewa leo na Mkurugenzi wa Mawasiliano Ikulu, Zuhura Yunus imefafanua mabalozi waliopangiwa vituo vya kazi kuwa ni; Balozi Khamis Mussa Omar kuwa Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini China.

Omar anachukua nafasi ya Balozi Mbelwa Brighton Kairuki ambaye amehamishiwa London, Uingereza.

Balozi Ccaser Chacha Waitara kuwa Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Namibia. Bw. Waitara anachukua nafasi ya Balozi Dk. Modestus Kipilimba ambaye amestaafu.

Dk. Modestus Kipilimba

Balozi Dk. Benard Yohana Kibesse kuwa Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Kenya. Balozi Kibesse anachukua nafasi ya Balozi Dk. John Stephen Simbachawene ambaye amehamishiwa Kampala, Uganda.

Balozi aliyehamishiwa kituo: Balozi Mbelwa Brighton Kairuki Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Uingereza. Balozi Kairuki anachukua nafasi ya Balozi Dk. Asha- Rose Migiro ambaye amemaliza mkataba wake.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

ACT: Waongoza watalii wapate maslahi yao inavyostahili

Spread the loveCHAMA cha ACT-Wazalendo kimeitaka serikali kuhakikisha inasimamia maslahi stahiki ya...

Habari za SiasaTangulizi

Prof. Lipumba ajitosa kuviunganisha vyama vya siasa Burundi

Spread the love  MWENYEKITI wa Kituo Cha Demokrasia Tanzania (TCD), Prof. Ibrahim...

Habari za Siasa

Prof. Muhongo akomalia matumizi nishati jadidifu kuondoa uhaba wa umeme

Spread the love  MBUNGE wa Musoma Vijijini (CCM), Profesa Sospeter Muhongo, ameendelea...

Habari za Siasa

Kilosa yawa mfano wa kuigwa miradi ya Mwenge nchini

Spread the love  KIONGOZI wa Mbio za Mwenge Kitaifa Godfrey Mzava amezitaka...

error: Content is protected !!