Tuesday , 7 May 2024
Home Habari Mchanganyiko Taasisi ya Wajibika yaja na muarobaini malalamiko huduma duni za afya
Habari Mchanganyiko

Taasisi ya Wajibika yaja na muarobaini malalamiko huduma duni za afya

Spread the love

TAASISI ya Wajibika, imeanzisha mradi wa Afya Shirikishi mkoani Dodoma, wenye lengo la kuimarisha mifumo ya utoaji na upokeaji huduma za afya kupitia njia ya ushirikishaji. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dodoma … (endelea).

Mradi huo umeanzishwa mwishoni mwa Aprili 2023, huku mafunzo yake yakiendelea kutolewa kwa baadhi ya watoa na wapokea huduma za afya katika kata nne za Dodoma, ikiwemo Mkonze, Matumbuli, Ihumwa na Chang’ombe.

Akizungumza katika mafunzo kuhusu mradi huo, yaliyotolewa katika Kata ya Mkonze, Mratibu wa Mradi wa Afya Shirikishi, John Mwilongo, ametaja sababu za kuanzisha mradi huo akisema ni kuondoa malalamiko ya wananchi juu ya kutoridhishwa na huduma za afya zitolewazo katika vituo vya afya na hospitali.

“Tuliona kwa nini kunakuwa na malalamiko ya wananchi kwamba nimeenda hospitali huduma haziridhishi, tukaona tuje na mradi huu ili kupunguza manung’uniko hayo,” amesema Mwilongo.

Mwilongo amesema mradi huo una lengo la kuimarisha mifumo ya utoaji na upokeaji huduma za afya, pamoja na kutoa fursa kwa wananchi kujifunza kwa karibu namna vituo vya afya vinavyotoa huduma ili kupunguza manung’uniko yanayoweza kuepukwa.

Mwenyekiti wa Kamati ya Afya Kata ya Mkonze, Shadrack Lucas, amesema mafunzo yanayotolewa kupitia mradi huo yamesaidiwa kuweka uwazi na uwajibikaji katika utoaji huduma za afya kwa kuwa wananchi.

“Kabla hatujapata elimu hii tulikuwa hatujui vitu vingi lakini baada ya semina tuliyopata tumefahamu sisi wanajamii tunatakiwa vitu gani tuvijue na tuvifanyie kazi. Mfano zamani kulikuwa hakuna uwazi wa mapato na matumizi katika vituo vya afya lakini Sasa wameweka baada ya kuhoji,” amesema Lucas.

Baada ya mradi huo kuanza katika Kata ya Mkonze, unatarajiwa kwenda katika Kata nyingine nne zilizopangwa kunufaika na mradi huo.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

Mahakama yatoa uamuzi zuio dhidi ya Club House

Spread the loveMAHAKAMA Kuu ya Tanzania, Masjala Kuu jijini Dar es Salaam,...

Habari Mchanganyiko

GGML, OSHA yawanoa bodaboda 200 Arusha

Spread the loveZAIDI ya madereva bodaboda 200 wa jiji la Arusha wamepatiwa...

BiasharaHabari Mchanganyiko

Serikali kuwakopesha wajasiriamali 18.5bn/- kupitia NMB

Spread the loveSerikali imetenga kiasi cha Sh 18.5 bilioni kwa ajili ya...

AfyaHabari Mchanganyiko

Huduma za kibingwa zazinduliwa katika hospitali za halmashauri 184

Spread the loveSERIKALI imezindua huduma za matibabu za kibingwa katika hospitali 184...

error: Content is protected !!