Tuesday , 7 May 2024
Home Habari Mchanganyiko Kafulila awapa darasa wahariri kuhusu idara ya PPP
Habari Mchanganyiko

Kafulila awapa darasa wahariri kuhusu idara ya PPP

Spread the love

KAMISHNA wa Idara ya Ubia kati ya Serikali na Sekta Binafsi (PPP), David Kafulila amesema msukumo wa kuunda taasisi hiyo ulitokana na kuwepo kwa mikataba mibovu kati ya serikali na sekta binafsi. Anaripoti Gabriel Mushi …(endelea).

Kafulila ametoa kauli hiyo leo tarehe 16 Mei 2023, alipokutana na Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF), jijini Dar es Salaam kwenye kikao kilicholenga kueleza majukumu ya taasisi hiyo na mwelekeo wake.

“Sera mahsusi ya ubia ilianza 1996 kutokana na kuwepo kwa mikataba mibovu baina ya serikali na sekta binafsi.

“Kanuni iliundwa mwaka 2011, 2015 na kufanyiwa marekebisho mengine mwaka 2018, na sasa kuna marekebisho tena,” amesema Kafulila.

Kafulila amesema, PPP msingi wake ni kuondoa migogoro kati ya sekta binafsi na serikali ambayo ilikuwa ikitokea mara kwa mara.

Amesema, kutokana na umuhimu wa sekta binafsi, serikali lazima itafute njia ili kuhakikisha sekta hiyo inaondolewa vikwazo.

“Lazima serikali itafute njia ambazo inaweza kuhakikishia sekta binafsi inakuwa, ndio maana imekuwa ikifanya marekebisho ya sera yake mara kwa mara,” amesema Kafulila.

Amesema, ushirikiano kati ya serikali na sekta binafsi kwa kiwango kikubwa, unasaidia kupunguza msongamano, mvutano na migogoro kati ya sekta za serikali, pia kusaidia watu kupata huduma kwa uraisi na haraka zaidi.

Akizungumzia Tanzania na ujenzi wa miradi mikubwa, Kafulila amesema, bado Tanzania inayo nafasi nzuri ya kuendela na ujenzi wa miradi ya namna hiyo kulinganisha na nchi nyingi za Afrika.

“Katika nchi nyingi za Afrika Mashariki, Tanzania ipo vizuri kwenye kupima uzito wa deni, kwamba tuna afadhali.

“Kutokana na utafiti uliofanywa na Global Credit Agency Mwaka 2017, 2021, na 2022 katika kupima madeni ya nchi, tuko vizuri katika ukanda wa Afrika Mashariki na Kusini mwa Jangwa la Sahara,” amesema.

Akizungumza kwenye kikao kazi hicho, Mwenyekiti wa TEF, Deodatus Balile amesema, kuna umuhimu mkubwa wa kulinda sekta binafsi kwa kuwa ndio inaendesha uchumi wa nchi.

Amesema, ushirikiano kati ya serikali na sekta binafsi unapaswa kuimarishwa na kuondolewa vimelea vyovyote vya uadui.

“Ushirikiano kati ya PPP na serikali ni muhimu, ulinzi wa PPP ni muhimu kwa kuwa unakuza uchumi wa nchi,” amesema.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

Mahakama yatoa uamuzi zuio dhidi ya Club House

Spread the loveMAHAKAMA Kuu ya Tanzania, Masjala Kuu jijini Dar es Salaam,...

Habari Mchanganyiko

GGML, OSHA yawanoa bodaboda 200 Arusha

Spread the loveZAIDI ya madereva bodaboda 200 wa jiji la Arusha wamepatiwa...

BiasharaHabari Mchanganyiko

Serikali kuwakopesha wajasiriamali 18.5bn/- kupitia NMB

Spread the loveSerikali imetenga kiasi cha Sh 18.5 bilioni kwa ajili ya...

AfyaHabari Mchanganyiko

Huduma za kibingwa zazinduliwa katika hospitali za halmashauri 184

Spread the loveSERIKALI imezindua huduma za matibabu za kibingwa katika hospitali 184...

error: Content is protected !!