OPERESHENI ya kiuchunguzi inayofanywa na Serikali ya China kwa kampuni za kigeni imeibua wasiwasi kwa kampuni hizo na kupelekea kufunga biashara zao nchini humo, Imeripoti New York Times … (endelea).
Kampuni hizo ni pamoja na Mintz Group, Bain Capvision Partners.
Kwa mujibu New York Times, China imekuwa ikilenga makampuni mashuhuri ya ushauri na uhusiano wa kigeni kwa kuyaweka viziuzini.
Inaelezwa kuwa kampuni hizo zinafanyakazi ya ushauri kwa wafanyabiashara wa kigeni nchini China kwa kufanya kutathmini uwekezaji kabla ya uwekezaji.
Mwezi Machi mwaka huu, Waziri wa Biashara wa China, Wang Wentao alitoa ahadi ya kuondosha vikwazo kwa kampuni hizo ili kampuni za kigeni ziwekeze zaidi.
Mbali na usumbufu wa sera ya sifuri ya Covid 19 Biashara za Kimataifa zinazovishwa na mzozo wa kisiasa wa kijiografia kati ya Washington na Beijing uliongeza hatari na kulazimisha mashirika mengi ya kimataifa kuandaa mipango ya dharura kwa njia mbadala ya China za kibiashara China.
Ulengaji wa hivi majuzi wa makampuni ya ushauri na uhusiano wa kigeni kupitia uvamizi, kuwekwa kizuizini na kukamatwa kumezua wasiwasi kuhusu kufanya biashara nchini China.

Dan Harris Mwanasheria wa Seattle anayefanya kazi na kampuni za kigeni nchini humo, ameshauri kuwa ili biashara ya Beijing iendelee basi Rais Xi Jinping, kiongozi mkuu wa China, hana budi kuimarisha usalama kwa kampuni za kigeni.
Harris alisema kuwa idadi kubwa ya wafanyabiashara katika wiki za hivi karibuni wakitafuta njia za kupunguza uwepo wao nchini China.
Mmoja wa wateja wake, mtengenezaji wa samani wa Marekani, anashughulikia mpango wa kusambaza bidhaa zake kupitia kampuni ya kichina ili iweze kuwaondoa wafanyakazi wake wa kimarekani nchini humo.
Leave a comment