Tuesday , 7 May 2024
Home Gazeti Habari za Siasa ACT wazalendo wampa tano Samia kufufua mchakato Katiba mpya
Habari za Siasa

ACT wazalendo wampa tano Samia kufufua mchakato Katiba mpya

Katibu Mkuu wa ACT-Wazalendo, Ado Shaibu
Spread the love

CHAMA cha ACT Wazalendo kimeunga mkono na kuikaribisha kwa mikono miwili hatua ya Rais Samia Suluhu Hassan kumuagiza Msajili wa Vyama vya Siasa nchini kuitisha kikao maalum cha Baraza la Vyama vya Siasa nchini kwa ajili ya kutathmini utekelezaji wa mapendekezo ya Kikosi Kazi cha kuratibu maoni ya wadau kuhusu demokrasia ya vyama vingi nchini. Anaripoti Mwandishi Wetu …(endelea).

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa jana tarehe 7 Mei 2023 na Katibu Mkuu wa chama hicho, Ado Shaibu,  imekuwa ni rai ya chama hicho kuhitaji ratiba ya utekelezaji wa mapendekezo ya kikosi kazi.

Amesema wanatarajia kikao hicho kitapatiwa ratiba hiyo ambayo itahakikisha kuna Sheria Mpya ya Uchaguzi na Sheria Mpya ya Vyama vya Siasa kabla ya mwisho wa mwaka huu.

“Vilevile kuhakikisha kwamba mabadiliko ya Sheria ya Mabadiliko ya Katiba yanafanyika ili kuanza mchakato wa Katiba Mpya kwa kuundwa kwa Timu ya Wataalam (Committee of Experts) kana ilivyopendekezwa na kikosi kazi.

“Ni mategemeo ya Chama chetu kuwa Baraza la Vyama vya Siasa itakuwa ni sehemu ya maandalizi ya Mkutano wa Kitaifa ili kujadili mambo yaliyokwamisha mchakato wa Katiba wa 2014 na kupata mwafaka kwayo ili mchakato wa sasa usikwame,” amesema.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaTangulizi

Jacob, Malisa wapandishwa kizimbani kwa mashtaka ya uongo mitandaoni

Spread the loveMKURUGENZI wa Shirika la Haki, Godlisten Malisa na mwanachama wa...

BiasharaHabari za Siasa

Bunge laitaka Serikali kudhibiti ufisadi miradi ya mkakati

Spread the loveKAMATI ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu, imeitaka Serikali kuimarisha...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Wizara ya Uchukuzi yaomba kuongezewa bajeti na Bunge

Spread the loveWIZARA ya Uchukuzi imeliomba Bunge liidhinishe bajeti yake kwa mwaka...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Serikali kutafuta mwekezaji mwingine Bandari ya Dar es Salaam

Spread the loveSERIKALI inaendelea kutafuta mwekezaji mwingine atakayeendesha gati namba nane hadi...

error: Content is protected !!