Tuesday , 7 May 2024
Home Kitengo Maisha Elimu Shule ya Wasichana – Dk. Samia yamwagiwa Sh. 50 milioni za vitanda
Elimu

Shule ya Wasichana – Dk. Samia yamwagiwa Sh. 50 milioni za vitanda

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akizindua ujenzi wa shule ya wasichana ya mkoa wa Songwe Dk. Samia High School iliyopo kata ya Namole halmashauri ya Mji Tunduma
Spread the love

 

SERIKALI ya imetoa Sh. 50 milioni kwa Halmashauri ya Mji Tunduma kwa ajili ya ununuzi wa vitanda katika shule mpya ya sekondari ya wasichana ya Dk. Samia High School inayotarajiwa kufunguliwa Julai mwaka huu. Anaripoti Ibrahim Yassin, Songwe … (endelea).

Awali shule hiyo iliyoanza kujengwa Januari mwaka jana, ilipatiwa Sh. tatu bilioni na serikali kuu kwa ajili ya ujenzi huku halmashauri ya mji Tunduma kupitia mapato yake ya ndani ikitoa Sh. 65 milionkna kuifanya fedha ya ujenzi kuwa shulea hiyo kuwa zaidi ya Sh. tatu bilioni.

Akizungumzia hatua ya mradi huo leo tarehe 1 Mei 2023 Ofisa Elimu Sekondari Tunduma, Patricia Mbigili amesema ujio wa fedha hizo za mradi uliifanya ofisi ya mkurugenzi kuhaha kwa kuhakikisha ujenzi unakamilika kwa wakati.

Amesema baada ya hapo halmashauri ililazimika kuingia mkataba na wakandarasi wengine ambao walitumia watenda kazi wengi ambao walijenga usiku na mchana na sasa mradi umefikia asilimia 70 huku mabweni mawili na baadhi ya vyumba vya madarasa yakiwa hatua za umaliziaji.

“Tumepokea fedha Sh. 50 milioni za ununuzi wa vitanda vya kuanzia, tunatarajia mwezi wa saba kuchukua wanafunzi watakaoanza kidato cha tano kazi iliyopo ni kuhakikisha majengo yanayotakiwa yakamilike haraka,” amesema.

Mkurugenzi mtendaji wa halmashauri hiyo, Filimon Magesa amesema baada ya mapokea hayo walilazimika kufunga taa na kuchimba kisima kirefu cha maji kwa fedha za mapato ya ndani lengo ni kuhakikisha mafundi wanajenga usiku na mchana na hilo lilifanikiwa.

Baadhi ya wananchi katika halmashauri ya mji Tunduma wilayani Momba mkoani Songwe wameiomba serikali kupitia halmashauri ya mji huo, kufanya jitihada za haraka kuhakikisha ujenzi wa vyumba vya madarasa na mabweni unakamilika kwa wakati ili yaweze kutumika na kuhepuka hatari za ujauzito kwa wasichana.

Sophia Juma Mkazi wa Tunduma amesema shule hiyo imejengwa sehemu sahihi nje ya mji na kuwa wasishana wengi wataondokana na vishawishi vya wanaume kutokana na kusoma na kulala hapohapo shuleni,hali itakayotokomeza mimba na utoro uliopo kwa baadhi ya maeneo.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

ElimuHabari za Siasa

Serikali kuongeza wanufaika mikopo ya elimu ya juu

Spread the loveSERIKALI imesema itaongeza idadi ya wanufaika wa mikopo ya elimu...

ElimuHabari za Siasa

Serikali kufumua mitaala ya vyuo vikuu, ufundi stadi

Spread the loveSERIKALI inakusudia kufanya mapitio katika mitaala na programu za vyuo...

ElimuHabari Mchanganyiko

Chongolo aagiza TAKUKURU kuchunguza ujenzi wa bweni

Spread the loveMkuu wa Mkoa wa Songwe, Daniel Chongolo amemuagiza Kamanda wa...

ElimuHabari Mchanganyiko

Ugawaji taulo za kike watajwa kutokomeza utoro shuleni

Spread the loveBAADHI ya wanafunzi na walimu wa shule za sekondari mkoani...

error: Content is protected !!