Friday , 9 June 2023
Home Kitengo Maisha Elimu Wanakijiji waamua kujenga sekondari, wamuangukia Rais Samia
Elimu

Wanakijiji waamua kujenga sekondari, wamuangukia Rais Samia

Spread the love

 

WANANCHI wa Kijiji cha Wanyere, Wilaya ya Musoma Vijijini mkoani Mara, wamemua kuanza ujenzi wa shule ya sekondari kwa ajili ya kuwaondolea wanafunzi adha ya umbali mrefu kufuata elimu katika vijiji jirani. Anaripoti Mwandishi Wetu, Mara … (endelea).

Wakizungumza na waandishi wa habari hivi karibuni wakati wakiandaa eneo la ujenzi wa sekondari hiyo, wanakijiji hao wamemuomba Rais Samia Suluhu Hassan, pamoja na Mbunge wa Musoma Vijijini, Prof. Sospeter Muhongo, kuwaunga mkono katika ujenzi huo.

Judith Chibunu, mkazi wa Kijiji cha Wanyere, amesema wananchi wamemua kujenga shule hiyo baada ya watoto wao kukabiliwa na changamoto ya kutembea umbali mrefu kwenda vijiji vya jirani ambako Kuna shule.

“Tumeamua kufungua shule hii ili watoto Wetu wapate elimu bila changamoto, kwa Sasa wanalazimika kuvuka vijiji vitatu kufuata shule. Serikali ya Rais Samia ni sikivu tunaomba ituunge mkono ili shule hii ikamilike,” amesema Chibunu.

Kwa upande wake Kaimu Mtendaji wa Serikali ya Kijiji cha Wanyere, Hanifa Ibrahim, amesema mwitikio wa wananchi katika ujenzi wa shule hiyo ni mkubwa, hali inayoonyesha kwamba Wana dhamira ya dhati ya kuhakikisha watoto wao wanapata elimu Bora.

Mbunge wa Musoma Vijijini, Prof. Muhongo ameunga mkono juhudi za wananchi hao kwa kuchangia mifuko 100 ya saruji.

Taarifa ya ofisi ya Mbunge wa Musoma Vijijini, imesema lengo la ujenzi wa shule hizo kwa kutumia nguvu za wananchi ni kuhakikisha zinafunguliwa na kuanza kutoa huduma kuanzia Januari 2024.

Kijiji cha Wanyere kinafuata nyayo za vijiji vingine 67 vya Jimbo Hilo kujenga shule za sekondari kwa nguvu zao pamoja na misaada kutoka kwa wadau wa maendeleo, ili kutatua changamoto ya wanafunzi kutembea umbali mrefu kufuata shule zilizoko katika vijiji vya jirani, pamoja na mrundikano wa wanafunzi.

Ofisi ya Prof. Muhongo imetoa wito kwa wadau wengine wa maendeleo kutoa michango Yao ili kufanikisha ujenzi wa shule hizo pamoja na maabara za masomo ya sayansi.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Elimu

Wanafunzi wa St Joseph Dar wabuni Satellite

Spread the loveWANAFUNZI na wahadhiri wa Chuo Kikuu cha Mtakatifu Joseph cha...

Elimu

Serikali yatoa Sh. 573 mil. kukamilisha wa ujenzi sekondari ulioanzishwa na wanakijiji

Spread the love  SERIKALI kupitia Wizara ya Ofisi ya Rais-TAMISEMI, imetenga Sh....

Elimu

CBE yaja na kozi mpya 16 zikiwemo za ujasiriamali na uvumbuzi

Spread the loveChuo cha Elimu ya Biashara (CBE) kuanzia mwaka wa masomo...

Elimu

SUA kuhakikisha tafiti zinazofanywa zisiachwe kwenye makabati

Spread the love  MRATIBU wa utafiti na machapisho katika kurugenzi ya uzamiri,...

error: Content is protected !!