Tuesday , 30 April 2024
Home Habari Mchanganyiko Heche ataja sababu za kugombea tena uenyekiti mawakili vijana
Habari Mchanganyiko

Heche ataja sababu za kugombea tena uenyekiti mawakili vijana

Spread the love

MWENYEKITI wa Chama cha Mawakili Vijana, anayemaliza muda wake, Wakili Edward Heche, amejitosa kugombea Tena nafasi hiyo ili amalize aliyoyanzisha. Anaripoti Regina Mkonde, Dar es Salaam…(endelea).

Heche ametaja sababu hiyo Leo Jumatano, akizungumza na MwanaHALISI, kuhusu sababu za kuwania nafasi hiyo katika Uchaguzi Mkuu wa Chama Cha Mawakili wa Tanganyika (TLS), unaitarajiwa kufanyika Mei, 2023.

“Nagombea Tena ili kuhakikisha kuwa Yale yote niliyoyafanya mwaka Jana yanaendeles na kuimarika zaidi. Mfano kuendelea kuwaunganisha mawakili vijana na kutatua changamoto zao,” amesema Heche.

Wakili huyo kijana amesema kuwa, akichaguliwa kuendelea kuwa mwenyekiti, atashirikiana na Serikali pamoja na wadau Kwa ajili ya kutengeneza fursa za ajira Kwa wanaohitimu masomo.

“Nitatafuta fursa za msaada wa kisheria kwa kutafuta wahisani watakaotufadhili ili tuweze kuwa na kituo Cha msaada wa kisheria kila wilaya ama zilipo mahakama. Lengo ni kusaidia ushauri wa kisheria na kutatua na masuala ya kijamii. Kuishauri Wizara ya Katiba na Sheria kuzitaka kampuni za kisheria kutoa nafasi ya mafunxi kwa mawakili vijana,” amesema Heche.

Heche amesema lengo lake endapo atachaguliwa  tena kuwa na nyadhifa hiyo, ni kuhakikisha fedha za mfuko wa mawakili vijana zinaendelea kuongezeka, huku akiahidi kuendelea kutatua changamoto zao wakiwa katika utekelezaji wa majukumu yao.

“Nitaendelea kuwashirikisha mawakili vijana na taasisi kwa vikao vyote vinavyohusu makongamano na mijadala mbalimbali kwa kuangazia maslahi Yao,” amesema Heche.

Akielezea shughuli alizofanya katika muhula wake WA kwanza, Heche amesema aliimarisha mahusiano kati ya chama cha mawakili vijana na TLS   ili kutatua changamoto zao, pamoja na kuanzisha mfuko wa chama hicho pamoja na michango hatua iliyowezesha mfuko huo kuwa na fedha.

Heche amesema katika uongozi wake alifanikisha mawakili vijana kupata fursa za kuendeleza taaluma zao.

2 Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

7 wafa Ulanga, mbunge alia kutelekezwa na mawaziri, Tanroad

Spread the loveWatoto saba wamepoteza maisha na zaidi ya kaya 70 kukosa...

Habari Mchanganyiko

Bil 12.4 zimetumika ujenzi wa miradi wilaya ya Momba

Spread the love MKUU wa wilaya ya Momba mkoani Songwe Kennan Kihongosi...

AfyaHabari Mchanganyiko

Songwe katika mikakati ya elimu ya lishe kudhibiti udumavu

Spread the love  SERIKALI mkoani Songwe imejipanga kuendelea kutoa elimu ya lishe...

Habari Mchanganyiko

NBC yapata tuzo ya mwezeshaji bora wa mikopo serikali Afrika

Spread the loveBenki ya NBC imepata tuzo ya Mwezeshaji Bora wa Pamoja...

error: Content is protected !!