JUKWAA la Wahariri Tanzania (TEF) limetoa cheti cha utambuzi kwa Benki ya NMB kuwa moja ya wadhamini wakuu wa mkutano wa 12 wa jukwaa hilo ulioanza kufanyika jana tarehe 29 mkoani Morogoro. Anaripoti Mwandishi Wetu…(endelea).
Waziri wa habari, Mawasiliano na Teknolojia ya habari, Nape Nnauye akimkabithi Kaimu Meneja tawi la NMB Wami Paul Nyoni (kulia) Cheti cha shukrani wakati wa ufunguzi wa mkutano wa 12 wa mwaka wa kitaaluma wa wahariri wenye kauli mbiu ya “Sheria ya habari na maendeleo ya vyombo vya habari” unaofanyika mkoani Morogoro. Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri, Deudatus Balile (kushoto) na Makamu Mwenyekiti Jukwaa la Wahariri, Bakari Machumu (wapili kulia). Benki ya NMB ilishiriki kama mdhamini kwenye mkutano huo unaoendelea mjini Morogoro.
Akikabidhi cheti hicho kwa niaba ya TEF, Waziri wa Habati, Mawasiliano na Teknolojia, Nape Nnauye kwa Kaimu Meneja Tawi la NMB Wami, Paul Nyoni aliipongeza NMB kwa kuwa mmoja wa wadau muhimu wa sekta ya habari nchini.
Waziri wa habari, Mawasiliano na Teknolojia, Nape Nnauye (katikati) akiteta Jambo na Kaimu Meneja tawi la NMB Wami, Paul Nyoni baada ya kupokea Cheti cha shukrani wakati wa ufunguzi wa mkutano wa 12 wa mwaka wa kitaaluma wa wahariri wenye kauli mbiu ya “Sheria ya habari na maendeleo ya vyombo vya habari” unaofanyika mkoani Morogoro. Wapili kushoto ni Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri, Deudatus Balile na Makamu Mwenyekiti Jukwaa la Wahariri, Bakari Machumu (kulia kabisa). Benki ya NMB ilishiriki kama mdhamini kwenye mkutano huo unaoendelea mjini Morogoro.
Leave a comment