Wednesday , 24 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Ukaguzi wa CAG yabaini madudu ‘Plea Bargain’
Habari za Siasa

Ukaguzi wa CAG yabaini madudu ‘Plea Bargain’

Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), Charles Kichere
Spread the love

 

UKAGUZI Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) kuhusu fedha makubaliano ya washatakiwa na Ofisi ya Taifa ya Mwendesha Mashitaka umebaini dosari kadhaa ikiwemo ukiukwaji wa maadili na matumizi mabaya ya ofisi. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).

Akiwasilisha taarifa hiyo jana mbele ya Rais Samia Suluhu Hassan, CAG Charles Kicheere alisema fedha zilizotaifishwa ziliwekwa kwenye akaunti ya makubaliano ya Plea Bagain badala ya akaunti za utaifishaji mali.

Aidha alibainisha fedha taslimu zilizotaifishwa na kukabidhiwa hazina bila kupitia akaunti maalum za utaifishaji mali zilikadiriwa kuwa Sh 1.3 bilioni.

Alisema hakukuwa na daftari la utunzaji fedha (cash book) zinazotokana na makubaliano na kushindwa kutoa stakabadhi za mapokezi ya fedha zilizotaifishwa kama sehemu ya utambulisho wa mapokezi hayo.

Aliongeza kuwa mapungufu katika usimamizi wa mali zilizotaifishwa upelekea uchakavu na kuhatarisha usalama na mali zilizotaifishwa kutoorodheshwa kwenye daftari la Ofisi ya Mwendesha Mashtaka.

Aidha alibaini kutokuwepo kwa uthibitisho wa makabidhiano na Wizara ya Fedha na Mipango kwa mali zilizotaifishwa na malalamiko ya baadhi ya waathirika kwamba walionewa katika zoezi zima la kukiri na kufanya makubaliano.

“Ukaguzi maalum umebaini pia kukosekana kwa uwazi katika mchakato wa majadiliano baina ya Ofisi ya Taifa ya Mashtaka na washatakiwa na hakukuwa na uteuzi rasmi wa timu za kuendesha majadiliano katika ofisi ya Taifa ya Mashitaka,” alisema Kicheere.

Kutokana na hali hiyo CAG alipendekeza kuundwa kwa tume huru ya kuchunguza ukiukwaji wa maadili na matumizi mabaya ya ofisi ya umma katika mchakato wa makubaliano ya kukiri kosa na kutaifisha mali za watuhumiwa.

1 Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Mwekezaji amwaga bil. 39 kujenga viwanda 3 vya uchenjuaji

Spread the loveKampuni ya Mineral Access System Limited (MAST) inayoiwakilishwa kampuni ya...

Habari za SiasaTangulizi

Mpwa wa Magufuli mbaroni kwa kusambaza picha za utupu

Spread the loveJESHI la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam limewakamata...

Habari za Siasa

Serikali kuanzisha mradi wa Gridi ya maji ya Taifa

Spread the loveWaziri wa Maji, Jumaa Aweso amesema katika mwaka wa fedha...

Habari za SiasaTangulizi

Shibuda amlima waraka mzito Bulembo

Spread the loveMKONGWE wa siasa nchini, John Shibuda amemshukia kada maarufu wa...

error: Content is protected !!