Tuesday , 7 May 2024
Home Habari Mchanganyiko Wadau wauchambua muswada sheria ya habari “ muswada wa kupunguza adhabu”
Habari Mchanganyiko

Wadau wauchambua muswada sheria ya habari “ muswada wa kupunguza adhabu”

Nape Nnauye, Waziri wa Habari
Spread the love

 

WADAU wa Umoja wa Haki ya Kupata Habari (CoRI), wameuchambua Muswada wa Sheria ya Huduma za Habari ya 2016, uliowasilishwa bungeni jijini Dodoma hivi karibuni, huku wakisema maudhui yake yamejikita zaidi kupunguza adhabu. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).

Uchambuzi huo ulifanyika jana Ijumaa, katika kipindi cha Kipima Joto, kinachorushwa na kituo cha televisheni cha ITV.

Mjumbe wa CoRI, Deus Kibamba, ameuchambua muswada huo akisema kuwa, maeneo ambayo Serikali inapendekeza kurekebishwa na Bunge ni matatu na kwamba maeneo mengine yaliyobaki ni inapendekeza kupunguza adhabu.

“Yako mambo ambayo tulipendekeza lakini hayakuingia, mimi binafsi ninasema kwa uchache muswada unaoletwa kurekebishwa usingepungua vifungu 16, bahati mbaya ninavyoona masuala yanayorekebishwa ni maeneo kama matatu kulikobaki kote kunapunguza adhabu. Huu muswada ningeuita muswada wa kupunguza adhabu,” alisema Kibamba.

Aidha, Kibamba amemshukuru Rais Samia Suluhu Hassan, kwa uamuzi wake wa kuagiza sheria hiyo ifanyiwe marekebisho kwa kuwa itasaidia Serikali yake kutekeleza amri iliyotolewa na Mahakama ya Afrika Mashariki, ya kurekebisha vifungu vyake 16 kati ya 18.

“Wakati ule hatuzungumzi tuliamua kwenda mahakamani kulalamika, tukapeleka vifungu 18 tuliona vimekaa sivyo. Mahakama ilisikiliza ile kesi mwisho wa siku ilitoa hukumu ikasema katika vifungu 18 mnavyolalamikia viwili hamna haki ya kulalamikia,” alisema Kibamba na kuongeza:

“Tunamshukuru Rais Samia aliagiza sheria iweze kurekebishwa, ninavyomchukulia anaona hadi Mahakama ya Afrika Mashariki imeagiza kurekebishwa, isiporekebishwa unakiuka mkataba ulioanzisha Jumuiya ya Afrika Mashariki.”

Deudatus Balile, Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri (TEF)

Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF), Deodatus Balile, alisema kuna baadhi ya mapendekezo yaliyotolewa na wadau kwa ajili ya maboresho ya tasnia ya habari, yameachwa katika Muswada wa Sheria ya Huduma za Habari ya 2016, ikiwemo kinachotoa mamlaka kwa Serikali, kutoa maelekezo kwa vyombo vya habari kutoa taarifa.

Aidha, Balile alisema kuna baadhi ya vifungu ambavyo wadau waliishauri Serikali viondolewe, vimefanyiwa kazi, ikiwemo cha makosa ya kashfa kuwa jinai, kinachoipa mamlaka Serikali kuratibu matangazo na kinachoelekeza mitambo iliyochapisha kashfa kutaifishwa.

“Wakati mwingine tusiende kavu anayetusikiliza akaona hawa watu hawana shukrani, vipo vifungu vilirekebishwa, kashfa kugeuzwa jinai ni jambo tulikuwa tunalipinga lakini marekebisho yaliyopendekezwa kuondoa kashfa kuwa jinai. Katika kifungu cha 51 waliweka utaratibu wa mkurugenzi wa idara ya habari maelezo kuratibu matangazo wamependekeza kiondoke,”alisema Balile.

Balile alisema “ukienda kifungu cha 38 (3) kuna habari ambazo zina kinga, habari ukizungumza bungeni au mahakamani huwezi shtakiwa ikichapishwa, lakini kifungu kidogo bila kujali bahari ina kinga utashtakiwa, katika marekebisho haya kinaondolewa.”

“Ukienda kifungu cha 50 (4) ilikuwa mitambo iliyochapishwa kashfa inataifishwa, hiki nacho kinapendekezwa kuondolewa. Tunasema ni jambo jema,” alisema Balile.

Deus Kibamba

Naye Makamu Mwenyekiti wa Taasisi ya Vyombo vya Habari Kusini mwa Afrika, Tawi la Tanzania (MISATAN), James Marenga, alisema muswada huo ulipaswa kuwasilishwa bungeni peke yake, badala ya kuwasilishwa kupitia marekebisho ya sheria mbalimbali, ili upate muda wa kutosha kujadiliwa.
Kwa upande wake, Mkurugenzi Mtendaji wa Chama cha Wanahabari Wanawake Tanzania (TAMWA), Dk. Rose Reuben, alisema muswada huo kuwasilishwa bungeni kwa njia ya marekebisho ya sheria mbalimbali, kunapunguza uzito wa marekebisho ya sheria hiyo.

“Ingekuwa vizuri sheria (Muswada wa Sheria ya Huduma za Habari ya 2016) ikafanyiwa marekebisho peke yake kuliko kuchanganya na nyingine, hii inapunguza kuona umuhimu wa sheria sababu wabunge walitakiwa kujadili ikiwa yenyewe kifungu hadi kifungu. Kwa hali ilivyo muda wa kujadili utakuwa haupo yale ya msingi yatakuwa hayajabadilishwa, tutakuwa tumefanya kazi haina matunda,” alisema Dk. Reuben.

Hata hivyo, Balile aliwashauri wadau wa habari kuacha kulalamika kwamba muswada huo haujawasilishwa peke yake, bali waangalie wapi kwenye mapungufu kwa ajili ya kutoa mapendekezo juu ya namna ya kurekebisha.

“Katika hali ya sasa tulicho nacho ni muswada ulioletwa katika marekebisho ya sheria ndogondogo, tukiendelea kulalamika ingekuja peke yake haipo. Tunachoweza fanya kuangalia wapi kuna upungufu ili tutumie ulimi tujenge hoja ya nguvu ifanye walioko mbele yao kuona ukweli na waone manufaa yake,” alisema Balile.

1 Comment

  • @THINK/Dedication/Remember/DREAMS”@ EMPLOY/US THEM ALL – ALL TANZANIAN HAS JOB TO DO

    In 2021, the unemployment rate in Tanzania remained nearly unchanged at around 32.74 percent. With a decline of 0.04 percentage points, there is no significant change to 2020. Over the observed period, the unemployment rate has been subject to fluctuation.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

AfyaHabari MchanganyikoMakala & Uchambuzi

Kisukari cha mimba ni nini?

Spread the loveKisukari cha mimba ni aina ya kisukari kinachotokea kwa baadhi...

Habari Mchanganyiko

Mafunzo kwa bodaboda 395 yamkuna Meya Dodoma

Spread the loveNAIBU Meya wa Jiji la Dodoma, Asma Karama amepongeza mafunzo...

Habari Mchanganyiko

Samia aagiza huduma za dharura maeneo yaliyoathiriwa na kimbunga Hidaya

Spread the love   RAIS wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania, Samia...

Habari Mchanganyiko

Mahakama yatoa uamuzi zuio dhidi ya Club House

Spread the loveMAHAKAMA Kuu ya Tanzania, Masjala Kuu jijini Dar es Salaam,...

error: Content is protected !!