Friday , 3 May 2024
Home Habari Mchanganyiko Mabasi ya masafa marefu sasa lazima kuwa na madereva wawili
Habari Mchanganyiko

Mabasi ya masafa marefu sasa lazima kuwa na madereva wawili

Mabasi yakiwa kituo cha mabasi Mbezi
Spread the love

 

WAZIRI Mkuu nchini Tanzania, Kassim Majaliwa, ameliagiza Jeshi la Polisi nchini humo kuhakikisha wanakagua mabasi yote ya masafa marefu na kujiridhisha kuwa yana madereva wawili. Anaripoti Mwandishi Wetu, Mwanza…(endelea).

Majaliwa ametoa agizo hilo leo Jumanne tarehe 14 Machi, 2023 wakati akizindua Wiki ya Nenda kwa Usalama Barabarani inayofanyika kitaifa mkoani Mwanza.

Majaliwa amesema uchunguzi unaonesha kuwa mabasi hususani yanayoenda mikoani na safari ndefu, ni miongoni mwa wahanga wakubwa wa ajali za barabarani kwasababu yakutofuata kanuni.

Amesema taratibu zilizowekwa na usalama barabarani ni mabasi hayo kuwa na madereva wawili ili kupokezana.

“Kumpa dereva mmoja aendeshe kutoka Dar es Salaam hadi Mwanza huo ni uzembe na hivyo basi nilielekeze jeshi la polisi na wasimamizi wengine wa sheria haya makampuni yanayokwenda umbali mrefu lazima yawahakikishie kuwa yana dereva zaidi ya mmoja ambao wataendesha kuelekea huko wanakokwenda kwa safari ndefu,” amesema Majaliwa.

Aidha amewataka wamiliki wa mabasi nao wahakikishe basi la mbali mrefu linakuwa na dereva zaidi ya mmoja.

“Serikali kwa upande wetu tutaendelea kuboresha miondombinu lengo hapa ni kukuza shughuli za usafirishaji ziwe nzuri Zaidi, mnaonunua magari yaendelee kuwa na hali nzuri,” amesema.

Majaliwa ametaja sababu zinazosababisha ajali kuwa ni pamoja ni watu kuendesha bila kuwa na mafunzo wala leseni ya kuendesha vyombo vya moto, kubeba abiria zaidi ya mmoja kwenye pikipiki, kutumia vilevi na kuendesha vyombo vya moto, kutumia simu, kuzidisha mizigo au abiria zaidi ya uwezo wa chombo chenyewe.

Amesema hivi sasa jeshi la polisi linakwenda kuimarisha usimamizi kuanzia kwenye vyuo vya kujifunza udereva, “kwahiyo kila mkoa najua vyuo hivyo vipo endeleeni kukaa pamoja na jeshi la polisi na hakikisheni mnatengeneza madereva wazuri.”

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Chadema waendelea kulilia katiba mpya

Spread the loveCHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimeendelea kudai upatikanaji wa...

BiasharaHabari Mchanganyiko

NMB yang’ara maonesho OSHA

Spread the loveBenki ya NMB imebeba tuzo ya kampuni bora kwenye sekta...

Habari MchanganyikoKimataifa

Ruto amteua Kahariri kuwa mkuu wa majeshi

Spread the loveRAIS wa Kenya, William Ruto, amemteua Jenerali Charles Muriu Kahariri,...

Habari Mchanganyiko

Chongolo aonya viongozi vijiji kutouza NIDA kwa wageni

Spread the loveMKUU wa Mkoa wa Songwe, Daniel Chongolo amewaonya viongozi wa...

error: Content is protected !!