Tuesday , 7 May 2024
Home Habari Mchanganyiko Papa Francis atimiza miaka 10 ya uongozi
Habari Mchanganyiko

Papa Francis atimiza miaka 10 ya uongozi

Papa Francis
Spread the love

 

KIONGOZI mkuu wa Kanisa Katoliki duniani, Papa Francis, leo Jumatatu anaadhimisha miaka 10 tangu alipochaguliwa kuliongoza kanisa hilo duniani.

Papa Francis, mwenye umri wa miaka 86, na raia wa Argentina, alikuwa papa wa kwanza kutoka Amerika ya kusini tarehe 13 Machi 2013, akimrithi Benedict XIV aliyestaafu na kufariki dunia mwishoni mwa mwaka jana.

Kardinali huyo wa zamani Jorge Mario ameamua kukuza maisha ya unyenyekevu katika uongozi wake.
Hakuwahi kuchukua makazi ya kipapa yaliyotumiwa na watangulizi wake.

Badala yake alisema anapendelea kuishi katika mazingira ya jamii kwa afya yake ya kisaikolojia.

Matatizo ya mara kwa mara ya goti yamemlazimisha kutumia mkongojo au kiti cha magurudumu, lakini hali yake ya afya inaonekana kuwa sawa.

Mei mwaka uliopita, aliripotiwa kumwambia msaidizi wake kwamba huliongozi kanisa kwa kutumia goti, bali kwa kutumia kichwa.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

Mahakama yatoa uamuzi zuio dhidi ya Club House

Spread the loveMAHAKAMA Kuu ya Tanzania, Masjala Kuu jijini Dar es Salaam,...

Habari Mchanganyiko

GGML, OSHA yawanoa bodaboda 200 Arusha

Spread the loveZAIDI ya madereva bodaboda 200 wa jiji la Arusha wamepatiwa...

BiasharaHabari Mchanganyiko

Serikali kuwakopesha wajasiriamali 18.5bn/- kupitia NMB

Spread the loveSerikali imetenga kiasi cha Sh 18.5 bilioni kwa ajili ya...

AfyaHabari Mchanganyiko

Huduma za kibingwa zazinduliwa katika hospitali za halmashauri 184

Spread the loveSERIKALI imezindua huduma za matibabu za kibingwa katika hospitali 184...

error: Content is protected !!