Saturday , 20 April 2024
Home Habari Mchanganyiko Saba wadaiwa kupoteza maisha kwa kula kasa Mafia
Habari Mchanganyiko

Saba wadaiwa kupoteza maisha kwa kula kasa Mafia

Spread the love

 

WATU saba wanadaiwa kupoteza maisha kisiwani Mafia, mkoani Pwani baada ya kula samaki aina ya kasa anayedaiwa alikuwa na sumu. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).

Akizungumza na MwanaHALISI Online kwa njia ya simu leo Jumatatu tarehe 13 Machi 2023, Mwenyekiti wa Serikali ya Kijiji cha Bweni, Juma Khamis, amethibitisha kutokea kwa vifo hivyo na kwamba watu wengine wanane wanaendelea kupatiwa matibabu katika vituo mbalimbali vya afya visiwani humo.

Khatibu amesema tukio hilo lilitokea Jumamosi tarehe 11 Machi 2023, ambapo miongoni mwa watu saba waliofariki, sita ni wakazi wa Kijiji cha Mbweni na mmoja ni kutoka kijiji jirani cha Kanga.

“Mpaka sasa hali ni shwari watu watatu wapo Hospitali ya Wilaya ya Mafia na wengine watatu wanauguzwa kwenye Zahanati ya Kirongwe wawili wapo Zahanati ya Bweni kwa ajili ya matibabu,” amesema Khatibu.

Mwanjuma Abdallah, mkazi wa Bweni Mafia akizungumza na MwanaHALISI kwa njiaya simu amesema kuwa yupo kwenye Zahanati ya Kirongwe anawauguza watoto wawili wa Juma Mitemba ambao mama yao alifariki kwa kula samaki huyo.

“Nipo zahanati hapa nawauguza watoto wa Mitemba mama yao alifariki jana kwa tatizo hilo hilo,” amesema.

Amesema kuwa Jumamosi ya tarehe 11 Machi 2023 katika kijiji cha Bweni kulikuwa na majonzi na simanzi ya kupoteza watu sita wa kijiji kimoja.

“Juzi tulipoteza watu sita kwenye kijiji chetu kulikuwa na makiwa kama ujavyo kijiji kizima ni ndugu wamoja kwa hivyo tumepoteza ndugu zetu,” alisema Mwajuma kwa sauti ya huzuni.

Mtandao huu ulipomtafuta kwa njia ya simu Kamanda wa Polisi Wilaya ya Mafia, alijibu kuwa hawezi kuzungumzia suala hilo kwa njia ya simu na kumtaka mwandishi afike visiwani humo ili kupata taarifa hiyo.

Naye Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Wilaya ya Mafia alipotafutwa alisema kuwa hawezi kuzungumzia jambo hilo hadi apate ruhusa kutoka kwa Kamanda wa Polisi wa Wilaya hiyo.

Hili si tukiola kwanza la watu kupoteza maisha kwa kula samaki aina ya kasa kwani itakumbukwa Novemba 2021 watu saba walifariki dunia visiwani Zanzibar na kusababisha Kamanda wa Polisi Mkoa wa Pemba Kaskazini, Juma Sadi kupiga marufuku ulaji wa samaki huyo.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

Gardner Habash wa Clouds Fm afariki dunia

Spread the loveALIYEKUWA mtangazaji wa kipindi cha Jahazi kinachorushwa na kituo cha...

BiasharaHabari Mchanganyiko

Wauguzi, madaktari 1000 kugawiwa mitungi ya Oryx Gas

Spread the loveKAMPUNI ya Oryx Gas na Taasisi ya Doris Mollel Foundation...

Habari Mchanganyiko

Tanzania yachaguliwa Makamu wa Rais Tume ya Shirika la Hali ya Hewa Duniani

Spread the love  TANZANIA kupitia Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA)...

Habari Mchanganyiko

NEMC yaonya wanaojenga bila tathmini ya mazingira

Spread the loveBARAZA la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC),...

error: Content is protected !!