Tuesday , 30 April 2024
Home Habari Mchanganyiko GGML yaahidi kuendelea kushirikiana na serikali, yachangia 40% mapato ya dhahabu
Habari Mchanganyiko

GGML yaahidi kuendelea kushirikiana na serikali, yachangia 40% mapato ya dhahabu

Spread the love

KAMPUNI ya Geita Gold Mining Limited (GGML) imeeleza kuridhishwa na juhudi za Rais Samia Suluhu Hassan kuvutia wawekezaji na kuboresha sekta ya madini  na kuifanya kampuni hiyo kuendelea kukua kila mwaka.

Pia imeahidi kuendelea kushirikiana na serikali kuhakikisha lengo la mchango wa sekta ya madini kufikia asilimia 10 ya pato ghafi la Taifa linafikiwa mwaka 2025 licha ya kwamba sasa limefikia asilimia 9.2. Anaripoti Mwandishi Wetu…(endelea).

Kauli hiyo imetolewa jana na Makamu Rais wa Kampuni mama ya GGML, AngloGold Ashati – anayeshughulikia miradi endelevu Ghana na Tanzania, Simon Shayo wakati akizungumza kwa niaba ya wadau wa sekta ya madini katika madahalo wa miaka miwili ya Rais Samia madarakani.

Makamu Rais wa Kampuni mama ya GGML, AngloGold Ashati – anayeshughulikia miradi endelevu Ghana na Tanzania, Simon Shayo akielezea mchango wa GGML katika mdahalo wa miaka miwili ya Serikali ya awamu ya sita madarakani chini ya Rais Samia Suluhu Hassan. Mdahalo huo umefanyika juzi mjini Geita.

Shayo alitolea mfano kuwa ripoti za karibuni kutoka Taasisi ya Uhamasishaji Uwazi na Uwajibikaji katika Rasilimali za Madini, Mafuta, na Gesi Asilia (TEITI) zinaonesha GGML inachangia kati ya asilimia 30 na 40 ya mapato yote au dhahabu yote inayouzwa kwa sekta ya madini Tanzania.

“Kwetu hiyo ni faraja na hapa Geita tunaamini kwa kushirikiana na serikali ya mkoa na halmashauri yetu na wilaya zetu tunaweza kuufanya mgodi wetu ukazalisha zaidi na wakati wote mgodi uendelee kuzalisha zaidi ya wakia 500,000 kwa mwaka,” alisema.

Aidha, alisema wanaamini sekta madini inaweza kuvuka malengo yaliyowekwa na Serikali iwapo wawekezaji pamoja na wachimbaji wadogo wataendelea kujengewa mazingira bora ya uwekezaji.

Mkuu wa Mkoa wa Geita, Martin Shigela

“Tunaendelea kuiomba serikali chini ya uongozi wa Rais Samia kuendelea kutuwekea mazingira mazuri, tunaahidi kuongeza  tija kwenye migodi yetu na sisi AngloGold Ashanti kupitia mgodi wetu wa GGML tunaamini wakati wote tutaendelea kuwa sehemu kubwa ya mafanikio hayo ya sekta ya madini,’ alisema.

Alisema uwepo wa GGML Tanzania, unajitafsiri si tu kwenye uchimbaji wa dhahabu na ulipaji wa kodi lakini kwenye uwekezaji kwenye jamii.

“Tunu yetu kubwa ni kwamba jamii ionekane kunufaika kwa sisi kuwepo hapa, tumejitahidi kwa uwezo wetu tangu tumeanza uchimbaji mjini Geita mwaka 2000 lakini tangu tumeanza kuingia makubaliano na halmashauri zetu kwa maana utekelezaji wa mpango wa CSR.

Mwanasheria Mkuu wa Kampuni uya Geita Gold Mining Limited (GGML) David Nzarigo (katikati) akimtambulisha Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa GGML, Wayne Louw (kulia) kwa Kamanda wa Polisi mkoani Geita, Safia Jongo

“Uwajibikaji wetu kwa jamii kupitia mpango ambao unasainiwa kwa pamoja tangu mwaka 2017, tumewekeza kila mwaka kati ya Sh bilioni 9.2. hadi 9.5 na mwaka huu tunaamini tutapata fursa ya kuunganisha mipango miwili ya mwaka 2022 na 2023 ambapo kwa wilaya ya Geita peke yake tutawekeza kiasi cha Sh bilioni 18.4,” alisema.

Alisema uwajibikaji wa GGML kwa jamii, unajitafsiri katika elimu, afya na kipato.

Aidha, alitoa ombi kwa Serikali kuendelea kuhakikisha wanachokifanya kwa jamii kinaongeza tija kusaidia serikali kupiga hatua zaidi kwenye huduma za jamii kwa wananchi wanaozunguka mgodi kunufaika.

Akizungumza katika mdahalo huo, Mkuu wa mkoa wa Geita, Martin Shigela alisema mkoa huo ndio namba moja kwa uzalishaji wa madini ya dhahabu kwani asilimia  60 ya mapato ya Taifa inatoka kwenye madini.

Alisema kwa miaka miwili iliyopita, wachimbaji wadogo na wakati wamezalisha kilo 13,000 sawa na tani 13.5 wakati migodi mikubwa kama GGML imezalisha kilo 35,000 sawa na tani 35.

“Mchango wetu katika kipindi cha miaka miwili unaonesha kuwa ardhi ya mkoa huu ina thamani ya Sh trilioni tano ambayo ni sawa na robo ya bajeti ya Taifa,’ alisema.

Alisema kwa kipindi cha miaka miwili, zaidi ya Sh bilioni 400 zimekusanywa kama mapato katika migodi inayochimba dhahabu Geita.

“Ukiangalia miaka ya nyuma hata asilimia 50 ya fedha ilikuwa haijafikiwa. Rais wetu amejenga mazingira uwekezaji, ametangaza nchi kimataifa na wawekezaji wanaweza kuja bila kuwa na hofu wala wasiwasi wowote,” alisema.

1 Comment

  • A. UTANGULIZI
    1. Mheshimiwa Spika, naomba kutoa hoja kwamba, Bunge lako Tukufu sasa lipokee na kujadili Taarifa ya Utekelezaji ya Mwaka 2022/23 na kupitisha Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya KUKU kwa Mwaka 2023/24.
    2. Mheshimiwa Spika, nianze kwa kumshukuru Mwenyezi Mungu, mwingi wa rehema kwa kuniwezesha kuwasilisha Hotuba hii muhimu mbele ya Bunge lako Tukufu. Aidha, kwa namna ya kipekee kabisa namshukuru Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kuniamini kuendelea kusimamia Sekta ya KUKU ili kufikia matarajio ya Watanzania katika Sekta ya KUKU ya kuongeza mchango wake kwenye Pato la Taifa.
    3. Mheshimiwa Spika, vilevile kwa dhati nampongeza Mhe. Rais kwa namna anavyoiongoza Serikali ya Awamu ya Sita inayosimamia utekelezaji wa Ilani ya uchaguzi ya Chama cha Mapinduzi (CCM) ya mwaka 2020-2025, ambapo mafanikio mengi yamepatikana katika sekta mbalimbali ikiwemo Sekta ya KUKU. Mafanikio hayo yameendelea kuitangaza nchi yetu siyo tu katika Bara la Afrika bali Duniani kote.
    4. Mheshimiwa Spika, ninaomba nitoe Rai kwa wananchi na Waheshimiwa Wabunge wote bila kujali itikadi za aina yoyote, tuendelee kuyaenzi mafanikio haya makubwa na kuendelea kushirikiana kwa pamoja katika kuchangia maendeleo ya kiuchumi na kijamii nchini.
    5. Mheshimiwa Spika, vilevile, nitumie fursa hii kuwapongeza na kuwashukuru Viongozi Wakuu wa Kitaifa, ambao ni Makamu wa Rais, Dr. Philip Isdor Mpango pamoja na Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dr Hussein Ali Mwinyi kwa hekima kubwa katika kumsaidia Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuongoza nchi yetu.
    6. Mheshimiwa Spika, pia, nimshukuru na kumpongeza Waziri Mkuu, Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa (Mb.) kwani amekuwa mstari wa mbele katika kusimamia na kufuatilia utekelezaji wa Ilani ya CCM na maelekezo mbalimbali ya Mhe. Rais pamoja na kusimamia vema shughuli za Sekta ya KUKU ndani na nje ya Bunge.
    7. Mheshimiwa Spika, ninakushukuru wewe binafsi, Naibu Spika, Wenyeviti wa Bunge, Wenyeviti wa Kamati za Kudumu za Bunge, akiwemo Kaimu Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya KUKU na YAO Mhe. TAN L. VIAZI (Mb.) na Wajumbe wa Kamati hiyo. Kamati hii imefanya kazi nzuri na kutoa ushauri wa kuboresha mambo mbalimbali ikiwemo kupitia na kuchambua Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya KUKU na Taasisi zake kwa mwaka 2022/23.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

7 wafa Ulanga, mbunge alia kutelekezwa na mawaziri, Tanroad

Spread the loveWatoto saba wamepoteza maisha na zaidi ya kaya 70 kukosa...

Habari Mchanganyiko

Bil 12.4 zimetumika ujenzi wa miradi wilaya ya Momba

Spread the love MKUU wa wilaya ya Momba mkoani Songwe Kennan Kihongosi...

AfyaHabari Mchanganyiko

Songwe katika mikakati ya elimu ya lishe kudhibiti udumavu

Spread the love  SERIKALI mkoani Songwe imejipanga kuendelea kutoa elimu ya lishe...

Habari Mchanganyiko

NBC yapata tuzo ya mwezeshaji bora wa mikopo serikali Afrika

Spread the loveBenki ya NBC imepata tuzo ya Mwezeshaji Bora wa Pamoja...

error: Content is protected !!