Friday , 3 May 2024
Home Gazeti Habari za Siasa ACT-Wazalendo yaiangukia Serikali kunusuru wananchi Liwale, Nachingwea
Habari za Siasa

ACT-Wazalendo yaiangukia Serikali kunusuru wananchi Liwale, Nachingwea

Spread the love

 

CHAMA cha ACT-Wazalendo, kimeitaka Serikali kuchukua hatua za haraka kuwasaidia wananchi wa wilaya za Liwale na Nachingwea mkoani Lindi, wanaokabiliwa na baa la njaa kutokana na mazao yao kuharibiwa na wanyama pori hususan Tembo wanaotoka Pori la Akiba la Selous. Anaripoti Mwandishi Wetu, Lindi … (endelea).

Wito huo umetolewa tarehe 2 Februari 2023 na Mwenyekiti wa ACT-Wazalendo mkoani Lindi, Isihaka Mchinjita, baada ya kufanya ziara katika vijiji vya Kata za Namapwiya, Mkoa, Kiparamnero na Mnero, wilayani humo na kubaini wanakabiliwa na baa la njaa.

“Tembo wametoka katika hifadhi ya Selous na kufanya uharibifu mkubwa wa mazao katika mashamba ya wananchi wa kwenye Kata za Namapwiya, Mkoka, Kiparamnero na Mnero zimeathirika sana tangu mwaka jana na hakuna fidia yoyote inayotolewa na mamlaka ya hifadhi hiyo,” alisema Mchinjita.

Mchinjita alisema “” Tulitarajia kwa hali ilivyo wananchi hao kupelekewa chakula cha msaada lakini mpaka sasa hakuna licha ya kuahidiwa kwamba wangepelekewa; ni wakati sasa Serikali iingilie kati kuwasaidia hawa wananchi kwa kuwapelekea chakula cha msaada.”

Akizungumzia sakata hilo, Katibu Tawala wa Wilaya ya Nachingwea, Omar Mwanga, amesema Serikali imeshaanza kuchukua hatua dhidi ya changamoto hiyo na kwamba imeanza kupeleka chakula kwa waathirika.

Katika hatua nyingine, Mchinjita alisema ataifikisha mahakamani Serikali endapo itashindwa kuwalipa fidia za wananchi waliouawa na Tembo pamoja na mazao yao kuharibiwa na wanyama yakiwa shambani.

Mchinjita aliyataja maeneo ya watu walioripotiwa kuuawa na tembo kuwa ni kata za Kibutuka, Milui, Kikulyungu, Makata, Mangilikiti, Mgongowele na Mlebwe.

Alisisitiza kwamba licha ya kuwapo hifadhi hiyo kubwa mkoani humo, hakuna mapato yoyote yanayoingia kwenye halmashauri zinazotunza na kupakana na hifadhi hiyo ya Selous.

“Mpaka sasa serikali haijalipa fidia kwa familia zilizopoteza ndugu na wapendwa wao waliouawa na tembo.

Mkoa wa Lindi una eneo lenye jumla ya kilometa za mraba 66000 na kati yake, kilometa za mraba 18000 ni hifadhi ya Pori la akiba la Selous ambalo ni sawa na asilimia 27 ya mkoa mzima wa Lindi.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Chadema waendelea kulilia katiba mpya

Spread the loveCHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimeendelea kudai upatikanaji wa...

Habari za SiasaTangulizi

Chadema kumshtaki Rais Samia

Spread the loveCHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimetishia kumfungulia kesi ya...

Habari za Siasa

Tume huru ya uchaguzi yatangaza uchaguzi mdogo Jimbo la Kwahani

Spread the love  TUME Huru ya Taifa ya Uchaguzi, imetangaza uchaguzi mdogo...

AfyaHabari za Siasa

Dk. Biteko aagiza utoaji huduma saratani usiwe wa kibaguzi

Spread the loveNaibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Doto Biteko...

error: Content is protected !!