Tuesday , 21 March 2023
Home Gazeti Habari za Siasa Vijana ACT-Wazalendo Dar wampa tano Rais Samia
Habari za Siasa

Vijana ACT-Wazalendo Dar wampa tano Rais Samia

Rais Samia Suluhu Hassan
Spread the love

 

NGOME ya Vijana ya Chama cha ACT-Wazalendo, kimempongeza Rais Samia Suluhu Hassan, kwa kuunda tume ya kuangalia namna ya kuboresha mfumo wa haki jinai nchini, kwa kuwa itasaidia kuondoa changamoto ya ubambikaji kesi kwa wananchi. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).

Pongezi hizo zimetolewa leo tarehe 3 Februari 2023 na Mwenyekiti wa Ngome ya ACT-Wazalendo Mkoa wa Dar es Salaam, Felix Kamugisha, ikiwa ni siku chache tangu Rais Samia azindue tume hiyo itakayofanya kazi kwa muda wa miezi minne kuanzia Februari hadi Mei mwaka huu.

“Tarehe 14 Januari 2023, kupitia kongamano la vijana wa Dar es Salaam, niliibua tabia ovu ya askari wetu kubambikia vijana kesi. Ahsante Rais kwa hatua ulioanza nayo kuutazama mfumo wa haki nchini,” amesema Kamugisha.

Rais Samia ameiagiza tume hiyo ipitie upya utendaji wa taasisi za haki jinai, ikiwemo mahakama, Jeshi la Polisi, Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Tanzania (TAKUKURU) na Ofisi ya Mkurugenzi wa Mashtaka nchini (DPP), ili kubaini changamoto zinazopelekea zishindwe kutekeleza majukumu yake kwa ufanisi, kwa ajili ya kuzitatua.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Rais Samia aagiza iundwe kamati ya pamoja ya Mawaziri mradi wa BBT

Spread the love  RAIS Dk. Samia Suluhu Hassan, amewaagiza mawaziri kuunda kamati...

Habari za Siasa

Rais Samia apangua makatibu tawala mikoa, ateua Kamishna DCEA

Spread the loveALIYEKUWA Kamishna wa Mamlaka ya Kudhibiti Dawa za Kulevya, Gerald...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

M/kiti bodi ya wadhamini Chadema afariki dunia

Spread the loveMWENYEKITI wa Bodi ya Wadhamini ya Chama cha Demokrasia na...

Habari za Siasa

Zitto: Nikifa Ado atavaa viatu vyangu

Spread the love  KIONGOZI Mkuu wa Chama cha ACT Wazalendo, Zitto Kabwe...

error: Content is protected !!