Friday , 26 April 2024
Home Habari Mchanganyiko TEF yawatuliza wadau wa habari marekebisho vifungu kandamizi
Habari Mchanganyiko

TEF yawatuliza wadau wa habari marekebisho vifungu kandamizi

Mwenyekiti wa TEF, Deodatus Balile
Spread the love

 

JUKWAA la Wahariri Tanzania (TEF), limewataka wadau wa habari nchini kuwa na subira kwa kuwa muswada wa mabadiliko ya Sheria ya Huduma za Habari ya 2016, utawasilishwa bungeni kwa ajili ya kufanyiwa kazi. Anaripoti Regina Mkonde, Dar es Salaam … (endelea).

Kauli hiyo imetolewa leo tarehe 3 Februari 2023 na Mwenyekiti wa TEF, Deodatus Balile, baada ya baadhi ya wadau kuhoji kwa nini ratiba ya vikao vya mhimili huo haijaweka wazi lini muswada huo utawasilishwa bungeni.

Balile amesema muswada huo haujawekwa kwenye ratiba moja kwa moja kwa kuwa, utawasilishwa bungeni kupitia marekebisho madogo ya sheria mbalimbali.

“Muswada utaingia bungeni katika kikao cha Bunge kinachoendelea sasa , nimetoa taarifa hii sababu nimeona watu wengi wanaangalia ratiba ya bungeni wananipigia simu vipi mbona haumo kwenye sheria zitakazojadiliwa. Lakini mimi nina taarifa za uhakika kwamba mpaka jana jioni kulikuwa na kila dalili kwamba utaingizwa bungeni,” amesema Balile na kuongeza:

“Isipokuwa kitakachobadilika nadhani hatutaona ule muswada kwa njia ya kawaida ambapo unapelekwa muswada unaojitegemea kama ilivyo kwa bima ya afya, kitakachotokea muswada utaingia katika utaratibu wa marekebisho madogo madogo ya sheria mbalimbali. Tuendelea kusubiria maana tunaendelea kuwasiliana na Serikali na watunga sera kuona jinsi gani itakavyokwenda.”

Hivi karibuni Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Nape Nnauye, alisema muswada huo uliolenga kufanya marekebisho dhidi ya vifungu vinavyolalamikiwa na wadau kuwa vinakandamiza uhuru wa tasnia hiyo, ulishindwa kuwasilishwa bungeni Novemba mwaka jana ili kutoa nafasi ya kutosha kupokea maoni ili ipatikane sheria bora zaidi.

Nape alisema kwamba mapendekezo ya wadau kuhusu marekebisho hayo yalifikishwa katika Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG), kwa ajili ya kupitiwa ili muswada wake uwasilishwe bungeni.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

Wakili: Ukimpa zawadi mwenza marufuku kumpora hata mkiachana

Spread the love  WANANDOA na watu waliko kwenye mahusiano ya kimapenzi, wamekumbushwa...

Habari Mchanganyiko

Majaliwa: Mvua zimesababisha vifo vya watu 155, kuendelea hadi Mei

Spread the love  WAZIRI Mkuu, Kassim Majaliwa amesema mvua kubwa za El-Nino...

Habari Mchanganyiko

Exim Bank yatoa  vitanda kwa shule ya Jeshi la Polisi Moshi

Spread the love  BENKI ya Exim imekabidhii  seti ya vitanda kwa Shule...

Habari Mchanganyiko

NBC yakabidhi vitanda Shule ya Polisi Moshi

Spread the loveBenki ya NBC imekabidhi msaada wa vitanda 28 kwa Shule...

error: Content is protected !!