Friday , 29 March 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Vigogo wanaokwamisha mradi Liganga na Mchuchuma kitanzani
Habari za SiasaTangulizi

Vigogo wanaokwamisha mradi Liganga na Mchuchuma kitanzani

Naibu Spika wa Bunge la Tanzania, Mussa Azan Zungu
Spread the love

 

NAIBU Spika wa Bunge, Mussa Zungu, watu wanaokwamisha utekelezaji wa mradi wa uchimbaji chuma cha Liganga na Makaa ya Mawe ya Mchuchuma, ulioko wilayani Ludewa, Mkoa wa Njombe, wachukuliwe hatua za kisheria. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dodoma … (endelea).

Zungu ametoa kauli hiyo leo Ijumaa, tarehe 3 Februari 2023, bungeni jijini Dodoma, baada ya Naibu Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Exaud Kigahe, kuueleza mhimili huo kuwa, majadiliano kati ya Serikali na muwekezaji wa mraid huo, yako katika hatua nzuri na kwamba yatakamilika mwaka wa fedha wa 2023/24.

“Waziri majibu hayo huu mwaka wa 10, kila mkija mnajibu hivyo hivyo na kama alivyosema mbunge kama siyo vita Ukraine makaa haya yasingekuwa na soko duniani. Yeyote wanaohusika mnaweza kuja kuwajibishwa kutokana na haya mambo mnayofanya,” amesema Zungu.

Kigahe alitoa kauli hiyo akijibu swali la Mbunge Viti Maalum, Neema Mgaya, aliyehoji lini Serikali itakamilisha majadiliano hayo ili mradi huo unaotarajiwa kutoa ajira rasmi 5,000 na zisizo rasmi zaidi ya 20,000, utaanza kwa kuwa baada ya miaka 15 makaa hayo yatakuwa hayana soko duniani.

Naibu huyo waziri alisema, Serikali imezamiria kuona mradi huo unganishi unatekelezwa mapema iwezekanavyo, na kwamba imefanya uthaminishaji mpya katika eneo la mradi baada ya ule wa kwanza kuisha muda wake. Amesema zoezi hilo lilikamilika Disemba 2022.

Kauli ya Zungu inakuja siku mbili tangu jambo hilo lilete mvutano mkubwa bungeni baada ya wabunge kupishana kuhusu mkataba na mwekezaji aliyepewa tenda hiyo, wakati wa wakijadili taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Viwanda, Biasharam na Mazingira ambayo ilieleza kilichokwamisha mradi huo kwa miaka 10.

Itakumbukwa kuwa tarahe 21 Septema 2011 Serikali iliingia makubaliano na kampuni ya Sichuan Hongda Group Corporation (SHG) baada ya kushinda mchakato wa tenda iliyoshindanisha kampuni 48 zilizoonesha nia.

Kwa mujibu wa taarifa ya Kamati ya Bunge, tangu kusaini kwa mkataba huo mradi haujawahi kutekelezwa hadi sasa kutokana na mwekezaji kutaka vivutio vya ziada vinavyolenga kumnufaisha zaidi kuliko maslahi ya Taifa.

Akichangia taarifa hiyo ya Kamati, Mbunge wa Kawe, Askofu Josephat Gwajima, alisema anashangaa kutotekelezwa kwa mradi wa Liganga na Mchuchuma licha ya kuwa ungeweza kuipatia Serikali kiasi cha Dola za Marekani 600 milioni hadi 1.5 bilioni kwa mwaka.

Gwajima aliongeza kuwa makubaliano baina ya Serikali na kampuni ya SHG yalisimamiwa na timu ya wataalamu wenye weledi kutoka Serikalini hivyo hakuna haja ya kutiliwa shaka kwa mkataba huo.

Gwajima alitaja waliounda timu hiyo kuwa ni pamoja na Kamishna wa Madini Kutoka Wizara ya Madini, Kaamishana wa Nishati kutoka Wizara ya Nishati na Madini, Mkurugenzi wa Viwanda kutoka Wizara ya Viwanda, Mkurugenzi wa Uendeshaji wa Shirika la Maendeleo ya Taifa (NDC), Kamishna wa Sera kutoka Wizara ya Fedha na Mchumi Mwandamizi Wizara ya Maendeleo na Miundombinu.

Wengine ni Mkurugenzi Msaidizi wa Mipango na Ukuaji kutoka Wizara ya Mipango naUezeshaji, Addoisa Mipango Mwandamizi Wizara ya Ardhi na Maendeleo ya Makazi, Mkurugenzi wa Mikataba ya Kimataifa kutoka Ofisi ya Mwanasheria wa Serikali, Mkurugenzi wa EPZA, Mkurugenzi Mtendaji wa TIC, Mkurugenzi Mkuu wa STAMICO, Mkurugenzi Mkuu wa TANESCO na Mkurugenzi Mkuu wa RAHACO.

Hata hivyo, Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Dk. Ashatu Kijaji alisema bungeni hapo kuwa tayari vyombo vya uchunguzi vimeanza kuichukunguza iliyokuwa kamati ya kitaalamu iliyoongoza majadiliano kati ya Serikali na mwekezaji huyo wani yalikuwa kinyume cha Sheria za nchi.

Alisema kutokana na mkanganyiko uliopo viongozi wakuu wa Serikali za awamu ya nne, tano na ya sasa waliagiza mikata hiyo kufuatiliwa.

“Ndiyo maana adendam iliyotolewa, GN haiwezi kutolewa kwasababu ipo kinyume cha Sheria za nchi hii.

Ndiyo maana wale wote waliokuwa kwenye timu mpaka sasa wapo kwenye vyombo vya uchunguzi vinafanya kazi kujiridhisha ni nini kilitokea mpaka hapo walipofikia,” alisema Dk. Kijaji.

Alisema lengo la uchunguzi huo ni kubaini nini kilitokea hadi kufikia makubaliano ambayo ni kinyume cha Sheria za nchi.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaMakala & Uchambuzi

Nani anasema kuna hasara ATCL?

Spread the loveRIPOTI za makusanyo na matumizi ya fedha katika Kampuni ya...

Habari za SiasaTangulizi

CAG: Wastaafu, wenza wao chanzo NHIF kufilisika

Spread the loveRIPOTI ya ukaguzi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu...

Habari za SiasaTangulizi

Vikundi hewa 851 vyalamba bilioni 2.6 mikopo ya halmashauri

Spread the loveVIKUNDI hewa vya wajasirimali wadogo 851 kutoka katika halmashauri 19...

Habari za SiasaTangulizi

Mashirika matano yapata hasara mabilioni ya fedha

Spread the loveMASHIRIKA matano ya Serikali yanayojiendesha kibiashara, yamepata hasara ya mabilioni...

error: Content is protected !!