Friday , 3 May 2024
Home Habari Mchanganyiko Takukuru yatangaza nafasi za ajira 320
Habari Mchanganyiko

Takukuru yatangaza nafasi za ajira 320

Spread the love

TAASISI ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) leo tarehe 21 Januari, 2023 imetangaza nafasi 320 za ajira kwa vijana wa Kitanzania wenye umri usiozidi miaka 30. Anaripoti Mwandishi Wetu …(endelea).

Kwa mujibu wa tangazo lililotolewa na Takukuru kupitia tovuti yao, nafasi hizo ni maofisa upelelezi nafasi 220 na nafasi 100 za wapelelezi wasaidizi daraja la tatu.

Aidha, taarifa hiyo imeeleza kuwa waombaji wa nafasi ya maofisa upelelezi wanatakiwa kuwa na Astashahada au shahada ya kwanza katika kozi ya uhandisi, usanifu, sayansi ya kompyuta, sheria, saikolojia na ushauri nasaha

Wakati katika nafasi ya wapelelezi wasaidizi daraja la tatu, wanaohitajika ni waliohitimu elimu ya sekondari na mafunzo yoyote yanayotambulika ikiwemo ya ufundi stadi kutoka katika taasisi zinazotambulika. Mwisho wa kutuma maombi ni Februari 10, 2023.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Chadema waendelea kulilia katiba mpya

Spread the loveCHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimeendelea kudai upatikanaji wa...

BiasharaHabari Mchanganyiko

NMB yang’ara maonesho OSHA

Spread the loveBenki ya NMB imebeba tuzo ya kampuni bora kwenye sekta...

Habari MchanganyikoKimataifa

Ruto amteua Kahariri kuwa mkuu wa majeshi

Spread the loveRAIS wa Kenya, William Ruto, amemteua Jenerali Charles Muriu Kahariri,...

Habari Mchanganyiko

Chongolo aonya viongozi vijiji kutouza NIDA kwa wageni

Spread the loveMKUU wa Mkoa wa Songwe, Daniel Chongolo amewaonya viongozi wa...

error: Content is protected !!