BENKI ya NMB imeingia makubaliano na Mamlaka ya Hifadhi Mji Mkongwe, chini ya usimamizi wa Wizara ya Utalii na Mambo ya Kale ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kuboresha bustani ya Forodhani. Anaripoti Mwandishi Wetu …(endelea).
Chini ya makubaliano hayo, Benki ya NMB itasimamia na kuhakikisha uwepo wa huduma na suluhishi za kifedha, elimu za kifedha na mikopo kwa wafanyabiashara wa Forodhani.
Itaweka maeneo maalum ya polisi, kubadilishia nguo wapiga mbizi na NMB Wakala.
Itaboresha maeneo ya kupiga mbizi Forodhani, na kutoa maboya kwa wapigambizi kwa ajili ya usalama wao sambamba na kuboresha taa zilizopo eneo la Forodhani.
Makubaliano haya yametiwa saini na Mkurugenzi wa Mamlaka ya Hifadhi Mji Mkongwe, Mhandisi Ali Said na Afisa Mkuu wetu wa Wateja Binafsi na Biashara – Filbert Mponzi huku wakishuhudiwa na Waziri wa Utalii na Mambo ya Kale, Simai Mohamed Said na viongozi wengine.
Leave a comment