Sunday , 5 February 2023
Home Gazeti Habari Mchanganyiko Takukuru yatangaza nafasi za ajira 320
Habari Mchanganyiko

Takukuru yatangaza nafasi za ajira 320

Spread the love

 

Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) leo tarehe 21 Januari, 2023 imetangaza nafasi 320 za ajira kwa vijana wa Kitanzania wenye umri usiozidi miaka 30. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dodoma … (endelea).

Kwa mujibu wa tangazo lililotolewa na Takukuru kupitia tovuti yao, nafasi hizo ni maofisa upelelezi nafasi 220 na nafasi 100 za wapelelezi wasaidizi daraja la tatu.

Aidha, taarifa hiyo imeeleza kuwa waombaji wa nafasi ya maofisa upelelezi wanatakiwa kuwa na Astashahada au shahada ya kwanza katika kozi ya uhandisi, usanifu, sayansi ya kompyuta, sheria, saikolojia na ushauri nasaha

Wakati katika nafasi ya wapelelezi wasaidizi daraja la tatu, wanaohitajika ni waliohitimu elimu ya sekondari na mafunzo yoyote yanayotambulika ikiwemo ya ufundi stadi kutoka katika taasisi zinazotambulika.

Mwisho wa kutuma maombi ni Februari 10, 2023.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoTangulizi

Haya hapa majina 12 ya familia moja waliofariki kwenye ajali Tanga

Spread the love  MAJINA 12 kati ya 17 ya waliofariki dunia katika...

Habari Mchanganyiko

Rais Samia awalilia 17 waliofariki ajalini wakisafirisha maiti

Spread the love  RAIS Samia Suluhu Hassan, ametuma salamu za rambirambi kwa...

Habari Mchanganyiko

Wanawake wachimbaji wajenga zahanati kuokoa afya za wakazi 2000

Spread the love  ZAIDI wakazi 2,000 wa kijiji cha Nyamishiga Kata ya...

Habari Mchanganyiko

Baada ya Congo DR, Somalia mbioni kujiunga na EAC

Spread the love  TAIFA la Somalia liko mbioni kuwa mwanachama rasmi wa...

error: Content is protected !!