Friday , 3 May 2024
Home Gazeti Habari Mandonga atimba Kenya na ngumi ‘Sugunyoo’ kutoka Ukraine
HabariMichezo

Mandonga atimba Kenya na ngumi ‘Sugunyoo’ kutoka Ukraine

Spread the love

 

BONDIA mcheshi nchini Karim Mandonga maarufu kama ‘Mtu Kazi’ amempiga mkwara mzito mpinzani wake Daniel Wanyonyi raia wa Kenya kwamba amekwenda na ngumi ya kigeni iliyozaliwa Ukraine kwenye midundo ya mabomu. Ngumi inayoitwa Sugunyoo. Anaripoti Mwandishi Wetu …(endelea).

Mandonga ametoa kauli hiyo leo tarehe 12 Januari, 2023 wakati akizungumza na waandishi wa habari nchini Kenya kuhusu pambano hilo linalotarajiwa kufanyika katika ukumbi wa KICC Jumamosi nchini humo.

Bondi huyo aliwasili nchini Kenya jana tarehe 11 Januari, 2023 kwa ajili ya maandalizi ya pambano hilo dhidi ya Wanyonyi linalosubiriwa kwa hamu

“Wanyonyi lazima tukupige tu! Unataka tunakupiga, hutaki tunakupiga! Hapa hapa Kenya,” amewaambia wanahabari.

Mandonga amebainisha kuwa yuko nchini humo kwa kubwa ya kumchapa mpinzani wake na baadaye anaweza kuchukua muda wa kubarizi.
“Toka nianze mchezo wangu wa Boxing, sijawahi kuahidi kwamba bondia nitampiga katika raundi ya ngapi, ila lazima apigike tu,” alisema.

Bondia huyo mwenye mbwembwe nyingi aliweka wazi kwamba yuko tayari kwa pambano lake dhidi ya Wanyonyi. Alimuonya mpinzani wa Kenya kuwa tayari kushindwa.

“Nimekuja na ngumi ya kigeni, ngumi iliyozaliwa Ukraine kwenye midundo ya mabomu. Ngumi inaitwa Sugunyoo,” alisema.
Mandonga amewashukuru mashabiki wake wa Kenya na wa Tanzania na kuwahakikishia ushindi katika pambano hilo la Jumamosi.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Michezo

Europa na Conference kukupatia pesa ndefu leo

Spread the love  ALHAMISI ya leo tutaenda kushuhudia mitanange ya kukata na...

Habari MchanganyikoMichezo

Wanamichezo Mei Mosi wachangia wahitaji vitu vya mil. 11.5

Spread the loveWanamichezo wanaoshiriki Michezo ya Mei Mosi Taifa 2024 jijini Arusha...

Michezo

Usiku wa Ulaya umerejea kibabe kabisa

Spread the love  LIGI ya Mabingwa barani Ulaya imerejea tena na awamu...

Habari MchanganyikoMichezo

Mambo ya Ndani, Ulinzi zang’ara michezo ya Mei Mosi Arusha

Spread the loveRais wa Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi nchini (TUCTA), Tumaini...

error: Content is protected !!