Tuesday , 7 May 2024
Home Habari Mchanganyiko Nape: Tusitumie mawasiliano kutapeli watu, kulaghai wanawake
Habari Mchanganyiko

Nape: Tusitumie mawasiliano kutapeli watu, kulaghai wanawake

Nape Nnauye, Waziri wa Habari, Mawasiliano na Tekinolojia
Spread the love

 

WAZIRI wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Nape Nauye amewataka Watanzania kutumia vizuri mawasiliano kujiajiri na kujiletea maendeleo badala ya kutapeli watu. Anaripoti Walter Mguluchuma, Katavi … (endelea).

Nape ametoa wito huo leo tarehe 10 Januari, 2023 wilayani Mlele mkoani Katavi wakati akizindua mnara wa mawasiliano uliojengwa na TTCL kwa kushirikiana na Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA).

Amesema Watanzania watumie uwepo wa mawasiliano hayo kujipatia ajira na si kudanganya watoto wadogo, na wanafunzi wa kike.
Nape amesisitiza kuwa wananchi watumie mawasiliano hayo kwa ajili ya maendeleo ya kilimo na biashara mbambali zitakazoweza wapatia fedha.

Amesema miradi hiyo ya minara imejengwa kwa fedha za walipa kodi hivyo ni mali ya wananchi wenyewe ambao pia wanajukumu la kuilinda na kuitunza.

Aidha, amesema Serikali inajua simu za kisasa gharama zake ni kubwa hivyo imeanza mazungumzo na watoa huduma mbalimbali wa mitandao waanzishe utaratibu kwa watu kupata simu za kisasa hata kwa mkopo na mazungumzo yanakwenda vizuri.

Mtendaji Mkuu wa Mfuko wa Mawasiliano kwa wote, Justina Mashiba amesema mamlaka hiyo inatekeleza shughuli zake kwa kuwa na miradi nchi nzima kwenye kila wilaya na mikoa.

“Mpaka sasa wameshirikiana na watoa huduma mbambali wa mawasiliano kama TTCL, Tigo, Vodacom, Airtel na makampuni mengine wameshasaini mikataba ya ujenzi wa minara 1,242 ya mawasiliano kwa nchi nzima na kati ya minara hiyo minara 1,087 imeshakamilika.

Amesema minara 155 iliyobaki ipo kwenye hatua mbambali za ukamilishwaji na itakapokuwa imekamilika na kufikia minara 1242 watakuwa wamewafikia Wanzania milioni 15.

Naye Mkurugenzi Mkuu wa TTCL, Peter Ulanga amesema Shirika hilo linaendelea kuboresha mawasiliano kwenye maeneo yote ambayo hayana mawasiliano yakiwepo maeneo ya mikoa ya pembezoni.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

Mahakama yatoa uamuzi zuio dhidi ya Club House

Spread the loveMAHAKAMA Kuu ya Tanzania, Masjala Kuu jijini Dar es Salaam,...

Habari Mchanganyiko

GGML, OSHA yawanoa bodaboda 200 Arusha

Spread the loveZAIDI ya madereva bodaboda 200 wa jiji la Arusha wamepatiwa...

BiasharaHabari Mchanganyiko

Serikali kuwakopesha wajasiriamali 18.5bn/- kupitia NMB

Spread the loveSerikali imetenga kiasi cha Sh 18.5 bilioni kwa ajili ya...

AfyaHabari Mchanganyiko

Huduma za kibingwa zazinduliwa katika hospitali za halmashauri 184

Spread the loveSERIKALI imezindua huduma za matibabu za kibingwa katika hospitali 184...

error: Content is protected !!