Sunday , 5 February 2023
Home Gazeti Habari za Siasa UVCCM: Vijana wafupi wasibaguliwe ajira Jeshi la Polisi
Habari za Siasa

UVCCM: Vijana wafupi wasibaguliwe ajira Jeshi la Polisi

MWENYEKITI wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM), Mohamed Ali Mohamedi, maarufu kama Kaiwada
Spread the love

 

MWENYEKITI wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM), Mohamed Ali Mohamedi, maarufu kama Kaiwada, amemuomba Rais Samia Suluhu Hassan, aondoe desturi ya Jeshi la Polisi kutoajiri vijana wafupi, akisema nao wana jukumu la ulinzi na usalama wa Taifa. Anaripoti Regina Mkonde, Dar es Salaam … (endelea).

Akizungumza katika hafla ya ufungaji wa matembezi ya UVCCM visiwani Zanzibar, leo tarehe 10 Januari 2023, Kawaida amesema kuwa Jeshi la Polisi limekuwa likiwapa kipaumbele cha ajira vijana warefu kuliko wafupi.

“Ombi la vijana wa Kitanzania kupitia kwenye Jeshi letu la Polisi, hatujui kama ni kanuni, utaratibu ama ni sheria yao ya kuwakataa vijana wenye asili ya ufupi na kuwaruhusu vijana wenye asili ya urefu. Huku ni kuonyesha kutukataa vijana ambao tuna asili ya ufupi na kuwapata kipaumbele vijana wenye urefu wakisahau kwamba jukumu la ulinzi na usalama wa taifa hili ni la vijana wote tukiwemo sisi wafupi,” amesema Kawaida.

Aidha, Kawaida amemshukuru Rais Samia kwa kuendelea kutoa ajira kwa vijana katika taasisi mbalimbali za Serikali ikiwemo ndani ya jeshi hilo.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Prof. Muhongo aungana na wananchi ujenzi maabara za sekondari

Spread the loveMBUNGE wa Musoma Vijijini, Profesa Sospeter Muhongo, kwa kushirikiana na...

Habari za Siasa

CCM apiga marufuku wazazi kuwatumia watoto wa kike kwenye mambo ya kimila

Spread the loveKATIBU Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Taifa Daniel Chongolo...

Habari za Siasa

Ofisi za mabalozi wa mashina zitumike kuwale vijana kimaadili – Chongolo

Spread the loveKATIBU Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Daniel Chongolo ameagiza...

Habari za Siasa

Vijana ACT-Wazalendo Dar wampa tano Rais Samia

Spread the love  NGOME ya Vijana ya Chama cha ACT-Wazalendo, kimempongeza Rais...

error: Content is protected !!