Friday , 3 May 2024
Home Kitengo Michezo Pele kuzikwa ghorofa ya 9 auone uwanja uliompa umaarufu
Michezo

Pele kuzikwa ghorofa ya 9 auone uwanja uliompa umaarufu

Spread the love

 

MFALME na muasisi wa soka la kisasa kutoka Brazil, mkongwe Pele aliyefariki wiki iliyopita atazikwa katika ghorofa ya 9 ya makaburi ya familia yenye ghorofa 14. Inaripoti Mitandao ya Kimataifa …(endelea).

Kulingana na taarifa kutoka Brazil, Pele alichagua kuzikwa katika ghorofa ya 9 ili kuendelea kutazama uwanja ambao ulimpa umaarufu katika mechi za ligi ya Brazil ambao ni uwanja wa timu ya Santos aliyoitumikia kwa muda mrefu na kupata umaarufu mkubwa maishani.

Mashabiki wake wanaojitolea wanaamini kwamba Pele ataweza kuona uwanja wake wa soka kwa milele.

Nyota huyo wa Brazil – mwanamume pekee katika historia kuwahi kushinda vikombe vitatu vya Dunia – alitumia muda mwingi kuchagua sehemu yake ya mwisho ya kuzikwa.

Pele atazikwa kesho Jumanne, huku shughuli za mazishi ikielezwa zitafanana na zile za Malkia. Uwanja wa Vila Belmiro, unaotumiwa na Santos FC, timu ambayo Pele alitumikia kwa sehemu kubwa ya maisha ya mpira ndiyo utatumika kwenye shughuli za mazishi leo Jumatatu na kesho Jumanne.

Santos historia yake haielezewi bila ya kumtaja Pele na ndiyo maana wamelichukua jukumu zima la mazishi yake.

Nyota mashuhuri wa kandanda wa Brazil atalala katikati ya uwanja wa Santos kwa saa 24, huku maelfu wakitarajiwa kutembelea jeneza lake kutoa heshima zao za mwisho.

Kisha mwili wake utaonyeshwa barabarani hadi Ecumenical Necropolis Memorial, ukisimama kwa muda mfupi katika nyumba ya mama yake aliyeko kitandani.

Pelé alichagua kumiliki ghorofa ya tisa ya jengo hilo mwaka wa 2003, kama njia moja ya kumuenzi baba yake aliyekuwa akivaa jezi namba 9 wakati akicheza.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Michezo

Europa na Conference kukupatia pesa ndefu leo

Spread the love  ALHAMISI ya leo tutaenda kushuhudia mitanange ya kukata na...

Habari MchanganyikoMichezo

Wanamichezo Mei Mosi wachangia wahitaji vitu vya mil. 11.5

Spread the loveWanamichezo wanaoshiriki Michezo ya Mei Mosi Taifa 2024 jijini Arusha...

Michezo

Usiku wa Ulaya umerejea kibabe kabisa

Spread the love  LIGI ya Mabingwa barani Ulaya imerejea tena na awamu...

Habari MchanganyikoMichezo

Mambo ya Ndani, Ulinzi zang’ara michezo ya Mei Mosi Arusha

Spread the loveRais wa Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi nchini (TUCTA), Tumaini...

error: Content is protected !!