Sunday , 5 February 2023
Home Kitengo Habari Kimataifa Prince Harry atamani kurudiana na baba, kaka yake
Kimataifa

Prince Harry atamani kurudiana na baba, kaka yake

Prince Harry
Spread the love

 

MWANAMFALME Harry anasema “Ningependa kurudiana na baba yangu, ningependa kuwa na kaka yangu,” kwenye utangulizi wa mahojiano kabla ya kutolewa kwa kumbukumbu zijazo za maisha yake. Yaameripoti Mashirika ya Kimataifa … (endelea).

Katika utangulizi wa mahojiano ya ana kwa ana na Tom Bradby wa ITV, anasema “hawajaonyesha kabisa nia ya kurudiana,” ingawa haijabainika anamuashiria nani.

Mwana Mfalame huyo pia alisema “alisalitiwa” kwenye kionjo cha mahojiano na shirika la utangazaji la Marekani CBS.

Buckingham Palace ilikataa kutoa maoni.

CBS na ITV zimetoa trela fupi pekee za vipindi vyao.

Mahojiano yote mawili yatapeperushwa tarehe 8 Januari, siku mbili kabla ya kumbukumbu ya maisha yake, Spare, kuchapishwa.

Katika trela za CBS, Prince Harry – Mtawala wa Sussex – anazungumza na mwandishi wa habari wa CBS 60 Minutes Anderson Cooper katika mazungumzo ambayo mtangazaji alielezea kama “milipuko”.

MwanaMfalme Harry anadai “alisalitiwa” pamoja na “maelezo, uvujaji na usingiziajii mambo dhidi yangu na mke wangu”.

Alisema: “Kauli mbiu ya familia ni ‘usilalamike kamwe, usielezee kamwe’, lakini ni kauli mbiu tu.

“Watalisha au kufanya mazungumzo na mwandishi, na mwandishi huyo atakuwa ameelekezwa namna ya kuandika taarifa hiyo, na chini yake, watasema wamefika kwenye Jumba la Buckingham kwa maoni.

“Lakini taarifa nzima ni maoni ya Buckingham Palace.”

“Kwa hiyo tunapoambiwa kwa miaka sita iliyopita, ‘hatuwezi kutia taarifa ya kukulinda’, lakini unafanya hivyo kwa wanafamilia wengine, inafika wakati ukimya ni usaliti.”

Prince Harry

Katika trela ya pili iliyotolewa na CBS, Prince Harry alisema hangeweza kujiona akirudi kwenye taasisi hiyo kutekeleza majukumu ya kifalme muda wote kama ilivyokua.

ITV ilisema mahojiano yake yataangazia uhusiano wa kibinafsi wa Prince Harry na “maelezo ambayo hayajawahi kutolewa” kuhusu kifo cha mama yake Diana, Princess wa Wales.

Mahojiano hayo yamerekodiwa mjini California ambako Harry na Mkewe wanaishi, mahojiano ya ITV pia yatamuonyesha Mwana Mfalme Harry akisimulia “kuvuja na kusingiziwa” mambo, kabla ya kuongeza: “Nataka familia, sio taasisi”. “Wanahisi kama ni bora kutuweka kama wahalifu,” anaongeza

Spare, ambayo inatarajiwa kutoa maelezo kuhusu tofauti kati yake na kaka yake Prince William, itaachiliwa mnamo Januari 10.

Mchapishaji Penguin Random House amekiita kitabu hicho “chapisho la kihistoria lililojaa ufahamu, ufunuo, uchunguzi wa kibinafsi na hekima iliyopatikana kwa bidii kuhusu nguvu ya milele ya upendo dhidi ya huzuni”.

Kitabu hiki kinafuatia kutolewa kwa waraka wa Netflix Harry na Meghan, ambapo Prince Harry alisema “ilikuwa hali ya kutisha” kuona kaka yake “akipiga kelele na kumkaripia” naye wakati wa mkutano wa kujadili mustakabali wa wanandoa hao katika Familia ya Kifalme.

Buckingham Palace ilikataa kutoa maoni kuhusu madai yaliyotolewa katika makala hayo.

Prince Harry na mke wake walielezea kwanini waliamua kuacha kazi ya kifalme na kuhamia Marekani, wakikosoa vyombo vya habari vya Uingereza na utendaji wa ndani wa taasisi ya kifalme.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Kimataifa

Papa Francis kukutana na wahanga wa vita Sudan Kusini

Spread the love  KIONGOZI wa Kanisa Katoliki Duniani Papa Francis leo Jumamosi...

Kimataifa

Polisi ahukumiwa kifo kwa kumuua wakili

Spread the love  MAHAKAMA kuu nchini Kenya imemhukumu kifo Ofisa wa Polisi,...

Kimataifa

Hospitali za China zilifurika wagonjwa, wazee kipindi cha wa likizo ya Mwaka Mpya wa Lunar

Spread the loveHOSPITALI  nchini China zimejaa wagonjwa na wazee katika kipindi cha...

Kimataifa

Papa Francis ayataka mataifa ya nje kuacha kupora mali DRC

Spread the love  KIONGOZI wa kanisa Katoliki Papa Francis, ameyataka mataifa ya...

error: Content is protected !!