Wednesday , 8 February 2023
Home Kitengo Habari Kimataifa Wakatoliki waanza kuuaga mwili wa Papa mstaafu Benedict
Kimataifa

Wakatoliki waanza kuuaga mwili wa Papa mstaafu Benedict

Spread the love

 

WAUMINI wa kanisa Katoliki leo tarehe 2 Januari, 2023 wameanza kutoa heshima zao mjini Vatican kwa papa mstaafu Benedict XVI, ambaye mwili wake umewekwa katika kanisa la Mtakatifu Petro kwa siku tatu kabla ya mazishi yake.

Kiongozi huyo wa kidini Mjerumani, aliyefariki dunia Jumamosi akiwa na umri wa miaka 95, aliliongoza kanisa katoliki kwa miaka minane kabla ya kuwa papa wa kwanza katika karne sita kujiuzulu mwaka wa 2013.

Mrithi wake Papa Francis ataongoza mazishi Alhamisi wiki hii katika uwanja mkubwa wa Mtume Petro, kabla ya mwili wake kuzikwa katika makaburi yaliyoko chini ya kanisa kuu la Mtume Petro.

Uongozi wa kanisa katoliki mjini Vatican ulitoa jana picha za maiti ya Benedict XVI, akiwa amevalishwa mavazi mekundu ya maombolezo ya upapa na akiwa na kilemba chenye ncha za dhahabu kichwani

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Kimataifa

Tetemeko la ardhi Uturuki: Vifo vyaongezeka hadi 4,800

Spread the love  Idadi ya vifo vilivyotokana na tetemeko lililotokea jana Jumatatu...

Kimataifa

Tetemeko la ardhi laua watu 300 Uturuki, Syria

Spread the love  WATU  300 wamefariki dunia katika tetemeko kubwa la ardhi...

Kimataifa

Urusi, Ukraine zabadilishana wafungwa wa kivita

Spread the loveJUMLA ya wafungwa 179 wa kivita wa Urusi na Ukraine...

Kimataifa

Papa Francis kukutana na wahanga wa vita Sudan Kusini

Spread the love  KIONGOZI wa Kanisa Katoliki Duniani Papa Francis leo Jumamosi...

error: Content is protected !!