Saturday , 27 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Dk. Samia aomba radhi kauli ya Mzee Makamba ‘wazuri hawafi’
Habari za SiasaTangulizi

Dk. Samia aomba radhi kauli ya Mzee Makamba ‘wazuri hawafi’

Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Rais Samia Suluhu Hassan
Spread the love

 

RAIS Dk. Samia Suluhu Hassan ambaye pia ni mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), amesema Katibu Mkuu mstaafu wa chama hicho, Yusuph Makamba aliteleza ulimi ndio maana akasema kwamba ‘wazuri hawafi’. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dodoma  …  (endelea).

Marekebisho hayo ya Rais Samia yamekuja siku moja baada ya mjadala mkali kuibuka miongoni mwa Watanzania katika mitandao ya kijamii kuhusu kauli ya Mzee Makamba alipomueleze Dk. Samia kuwa asiogope kufa kwa sababu wazuri hawafi.

Aidha, akitoa hotuba ya kufunga mkutano wa 10 wa chama hicho uliofanyika leo tarehe 8 Disemba, 2022 jijini Dodoma, Rais Samia ameongeza kuww Mzee Makamba alikuwa kwenye ‘emotion’.

“Katika dhana ya kujikosoa na kujisahihisha naomba kurekebisha ulimi ulioteleza wa kaka yangu Mzee Makamba kwamba wakati ananisifia alisema ‘usiogope hutokufa…mtu mzuri hafi.’

“Hajakusudia kwamba wanaokufa ni watu wabaya… wote hapa tumefiwa na baba na mama na ndugu, wote ni wapenzi wetu.
Kwa hiyo nirekebishe ili kipengele kile kisiende kutumika vibaya.

“Mzee alikuwa kwenye emotion, alidhani amenikosea aliponiambia si utakufa utatupisha! lakini akajirudisha akaniambia usijali mtu mzuri hafi. Alikuwa kwenye emotiona lakini hajakusudia vingine vyovyote,” amesema Rais Samia ambaye jana amechaguliwa rasmi kwa kupigiwa kura na wajumbe wa mkutano huo kuwa mwenyekiti wa kwanza mwanamke wa CCM.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Sauti ya Watanzania waeleza sababu za kuiunga mkono Chadema

Spread the love  KIKUNDI kinachojipambanua katika kupigania rasilimali na uhuru wa nchi,...

Habari MchanganyikoTangulizi

Jacob, Malisa waachiwa kwa masharti

Spread the love  JESHI la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam,...

Habari za SiasaKimataifaTangulizi

Tanzania, Somalia kuibua maeneo mapya ya ushirikiano

Spread the love  RAIS Dk. Samia Suluhu Hassan, amesema Tanzania na Somalia...

Habari za Siasa

ACT: Waongoza watalii wapate maslahi yao inavyostahili

Spread the loveCHAMA cha ACT-Wazalendo kimeitaka serikali kuhakikisha inasimamia maslahi stahiki ya...

error: Content is protected !!