Sunday , 29 January 2023
Home Gazeti Habari za Siasa Makundi CCM yamchefua Dk. Samia
Habari za Siasa

Makundi CCM yamchefua Dk. Samia

Kamati Kuu ya Chama cha Mapinduzi (CCM)
Spread the love

MWENYEKITI wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Taifa Rais Samia Suluhu Hassan amewataka wanachama wa chama hicho kuacha kujenga nyufa ndani ya chama baada ya chaguzi kukamilika. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dodoma … (endelea).

Dkt Samia ametoa kauli hiyo leo tarehe 8 Disemba, 2022 mkoani Dodoma katika siku ya pili na ya mwisho ya mkutano mkuu wa 10 wa CCM.

Amesema ndani ya CCM bado kuna makundi ambayo yanaendeleza nongwa hata baada ya kumalizika kwa chaguzi hizo.

Dk. Samia amesema makundi hayo hayajengi chama na badala yake yanakidhoofisha na kukifanya kushindwa kutekeleza majukumu yake kikamilifu.

Amesema anapenda kukiona Chama Cha Mapinduzi kikiendelea kuwa chama na chombo madhubuti cha kufuta unyonyaji wa aina zote na kupambana na jaribio lolote la uonevu.

Mwenyekiti huyo wa CCM Taifa pia amekumbusha majukumu ya chama hicho kuwa ni pamoja na kuisimamia serikali ili iweze kuwaletea maendeleo wananchi wake.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

NCCR-mageuzi yawaangukia Polisi kupotea kwa kada wake

Spread the loveJESHI la Polisi nchini limeombwa kufanya uchunguzi wa kina utakaosaidia...

Habari za Siasa

Uamuzi kesi ya kupinga Bodi ya Wadhamini NCCR-Mageuzi kutolewa Februari 6

Spread the love  MAHAKAMA Kuu, Masjala Kuu ya Dar es Salaam, imepanga...

Habari za SiasaTangulizi

Lissu:Suluhu ya ugumu wa maisha ni Katiba Mpya

Spread the love  MAKAMU mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo-Chadema Bara,...

Habari za Siasa

Lissu: Miaka 30 ya vyama vingi haikupambwa kwa marumaru

Spread the love  MAKAMU Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo-Chadema, Tundu...

error: Content is protected !!