Friday , 26 April 2024
Home Kitengo Maisha Elimu Serikali yaahidi kutatua changamoto za DMI
ElimuHabari

Serikali yaahidi kutatua changamoto za DMI

Spread the love
WIZARA ya Ujenzi na Uchukuzi imeahidi kuzifanyia kazi changamoto mbalimbali zinazokikabili Chuo ch bahari Dar es Salaam (DMI). Anaripoti Mwandishi Wetu…(endelea)

Ahadi hiyo ilitolewa jana na Naibu Waziri wa wizara hiyo, Atupele Mwakibete, wakati wa mahafali ya 18 ya chuo hicho ambapo wahitimu 904 walitunukiwa vyeti wakiwemo 11 wa Shahada za Uzamili.

Alisema anatambua jitihada kubwa zilizofanywa na chuo katika kukabiliana na changamoto mbali mbali ikiwemo suala la meli ya mafunzo, uhaba wa madarasa, ofisi, na vifaa vingine vya kufundishia zimekuwa changamoto sugu kwa chuo hiki.

“Kama hatua ya awali ya utatuzi wa changamoto husika, ningependa sasa kuishauri Menejimenti ya chuo iandae muhtasari ikibainisha changamoto na mapedekezo kuhusu namna gani bora Wizara  isaidie katika kumaliza changamoto zote kulingana na uharaka, uzito au athari za changamoto husika,” alisema.

 “Napenda kuwahakikishia kwamba, mara baada ya kupokea muhtasari wa changamoto hizo Ofisi yangu itazishughulikia mapema iwezekanavyo ili nanyi muweze kuboresha huduma zenu maana ni jukumu letu sote kwa pamoja kuhakikisha kwamba shughuli za bahari zinatekelezwa katika mfumo endelevu kwa lengo la kupata maendeleo endelevu kwa taifa letu kupitia uchumi wa bluu kama ambavyo imekuwa ikisisitizwa mara kwa mara na viongozi wakuu wa Serikali,” alisema Mwakibete

 Alitoa wito kwa wahitimu wakatumie ujuzi walioupata kwa manufaa yenu na manufaa ya taifa kwa ujumla na waweke maslahi ya taifa mbele wakitambua kuwa dhana ya uchumi wa bluu ni pana na ina fursa nyingi ikilinganishwa na sekta nyingine.

 “Nendeni mkachape kazi katika hatua yoyote inayofuata baada ya hapa mkatumie ujuzi mlioupata kama nyenzo muhimu katika kukuza uchumi wa nchi kupitia fursa zilizoko baharini na mkawe kivutio kwa vijana wenzenu wanaochipukia ili nao waone faida ya kusoma hapa DMI,” alisema.

 Aliwataka wasibweteke na elimu mliyoipata na badala yake wakajiendeleze zaidi ili hatimaye waweze kuwa wabobezi wa masuala ya bahari kwa ustawi wa taifa na dunia kwa ujumla.

Kaimu Mkuu wa Chuo cha Bahari Dar es Salaam (DMI), Dk. Tumaini Gurumo akizungumza kwenye mahafali ya chuo hicho ambayo yamefanyika leo chuoni hapo ambapo wahitimu 904 walipewa vyeti vyao wakiwemo 11 wa Shahada za Uzamili.

 “Ninaamini kwamba, mkiyazingatia hayo mtafanikiwa na hatimaye kuwa mabalozi wazuri wa Chuo chetu cha DMI mkikitangaza vyema ndani na nje ya mipaka ya Tanzania huku mkinufaika na ajira nyingi zinazohitaji vigezo ambavyo tayari sasa mnavyo yaani ujuzi, elimu na mafunzo ya bahari,” alisema .

Aidha, alisema kwa kuzingatia kuwa mchango wa sekta ya  usafirishaji wa shehena za kimataifa kwa njia ya bahari ndiyo muhimili wa uchumi wa dunia, Serikali ilipanua wigo wa majukumu ya chuo hiki ili kiwe chachu ya kukuza uchumi wa taifa letu kupitia matumizi sahihi ya vyanzo vya maji.

 Alisema hivi sasa kuna ongezeko zaidi la wataalam katika sekta ya bahari kutokana na nchi kutekeleza zana ya uchumi wa buluu.

 “Hii ina maana kwamba, wahitimu wa chuo hiki cha DMI ndio wanaotegemewa kwa kiasi kikubwa kuwa watenda kazi kwenye sekta ya bahari ikiwemo vyombo vya usafirishaji majini kama vile meli, uendeshaji na usimamizi wa bandari zetu, uchukuzi na lojistik, mafuta na gesi na usanifu na ujenzi wa meli,” alisema.

Mwenyekiti wa Bodi ya Chuo cha Bahari (DMI), Kapteni Ernest Bupamba akizungumza kwenye mahafali hayo ambayo yamefanyika leo chuoni hapo ambapo wahitimu 904 walipewa vyeti vyao wakiwemo 11 wa Shahada za Uzamili

 Alisema taaluma hizo zina mchango mkubwa katika ukuaji uchumi wa buluu na kwamba kwa msingi huu aliwapa changamoto  wahitimu wa DMI ya kuhakikisha ujuzi na elimu waliyopata hapa DMI inaenda sambamba na lengo la Serikali la kufanya kazi kwa weledi na umahiri  ili kujenga uchumi wa taifa letu kupitia sekta ya bahari.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

ElimuHabari za Siasa

MbungeCCM ataka kasi uzalishaji walimu ipunguzwe akidai hakuna ajira

Spread the love  MBUNGE wa Mlalo (CCM), Rashid Shangazi, ameishauri Serikali ipunguze...

ElimuHabari za Siasa

Walimu 52,551 kupandishwa madaraja mwaka huu

Spread the loveNaibu Waziri wa nchi, Ofisi ya Rais (Utumishi na Utawala...

BiasharaElimu

NMB yatoa vifaa vya ujenzi kwa shule sita Nyasa  

Spread the loveBENKI ya NMB imetoa msaada wa vifaa mbalimbali vya ujenzi...

ElimuHabari Mchanganyiko

GGML yawapa mbinu wanafunzi Geita Boys kufikia malengo ya kitaaluma

Spread the loveKampuni ya Geita Gold Mining Limited (GGML) imetoa mafunzo maalumu...

error: Content is protected !!