Friday , 26 April 2024
Home Habari Mchanganyiko TCRS, Serikali watoa elimu kuelekea siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia
Habari Mchanganyiko

TCRS, Serikali watoa elimu kuelekea siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia

Spread the love


KUELEKEA siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia Serikali kwa kushirikiana na Shirika la kikristo la kuhudumia wakimbizi nchini (TCRS) wametoa mafunzo ya kupinga ukatili wa kijinsia na kuwafikia watu 954 kwenye Tarafa ya Mikese Wilayani Morogoro. Anaripoti 
Christina Haule, Morogoro … (endelea).

Meneja wa TCRS Rehema Samwel alisema hayo jana wakati mafunzo hayo endelevu yakitolewa kwenye kata ya Tomondo wilayani humo ambapo kati ya watu hao 954 waliofikishiwa elimu hiyo wanaume ni 286, wanawake ni 332, watoto na vijana ni 317 na wenye ulemavu ni 19.

Alisema wamefanikiwa kutoa mafunzo kwa kamati za Ulinzi wa mama na Mtoto (MTAKUWA) kwa lengo la kuhakikisha jinsi gani wanakabiliana na kesi za ukatili dhidi ya mama na mtoto, pia wametoa mafunzo kwa wanafunzi mashuleni, vikundi vya ujasiriamali ikiwemo vijana, wanawake na watoto.

Samwel alisema mafunzo hayo ya kupinga ukatili wa kijinsia yamefanyika kwenye Tarafa ya Mikese katika kata za Mikese, Tomondo, Tawa na Kiroka yenye kauli mbiu isemayo ‘kila uhai una thamani-tokomeza mauaji na ukatili dhidi ya wanawake na watoto’.

Aidha Samwel alisema lengo la mafunzo hayo ni kuipa mwanga jamii juu ya madhara ya ukatili wa kijinsia na kujiweka tayari jinsi ya kuupinga kutokana na kuendelea kushika kasi katika maeneo na rika tofauti nchini na duniani kwa ujumla.

Hata hivyo Samwel aliihimiza jamii kuvunja ukimya ili kutokomeza suala zima la ukatili wa kijinsia kwa Wanawake, vijana wa kike na wa kiume kwa sababu bila kufanya hivyo wanaweza wakakumbana na hali ngumu katika kupambana na ukatili wa kijinsia baada ya kuota mizizi.

Aidha aliwataka wazazi kuwa na muda wa kuwasikiliza watoto wao tena kwa faragha ili kujua unyanyasaji dhidi yao unatokea wapi na kuweza kuwasaidia mapema.

Naye Afisa Ustawi wa jamii kata ya Tomondo Piencia Mushi akitoa mada ya unyanyasaji wa kijinsia kwa wanafunzi wa shule ya Sekondari Tomondo aliwasisitiza wanafunzi hao kuzingatia na kuitumia elimu ya kupinga ukatili wa kijinsia wanayopewa kwa lengo la kupambana na ukatili wa aina mbalimbali ambao una nafasi ya kuwarudisha nyuma katika maendeleo kielimu.

Mada zingine zinazoendelea kutolewa kwenye mafunzo hayo ni pamoja na utelekezaji wa watoto, ajira hatarishi, unyanyasaji wa kijinsia na ukatili wa kijinsia ukatili dhidi ya wanawake, ndoa za utotoni na madhara ya ndoa za utotoni.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

Wakili: Ukimpa zawadi mwenza marufuku kumpora hata mkiachana

Spread the love  WANANDOA na watu waliko kwenye mahusiano ya kimapenzi, wamekumbushwa...

Habari Mchanganyiko

Majaliwa: Mvua zimesababisha vifo vya watu 155, kuendelea hadi Mei

Spread the love  WAZIRI Mkuu, Kassim Majaliwa amesema mvua kubwa za El-Nino...

Habari Mchanganyiko

Exim Bank yatoa  vitanda kwa shule ya Jeshi la Polisi Moshi

Spread the love  BENKI ya Exim imekabidhii  seti ya vitanda kwa Shule...

Habari Mchanganyiko

NBC yakabidhi vitanda Shule ya Polisi Moshi

Spread the loveBenki ya NBC imekabidhi msaada wa vitanda 28 kwa Shule...

error: Content is protected !!