Thursday , 28 March 2024
Home Habari Mchanganyiko UNHCR yaadhimisha miaka 30 ya DAFI, wakimbizi 22,500 wanufaika
Habari Mchanganyiko

UNHCR yaadhimisha miaka 30 ya DAFI, wakimbizi 22,500 wanufaika

Spread the love

 

SHIRIKA la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Wakimbizi (UNHCR), limefanya maadhimisho ya miaka 30 ya Taasisi inayotoa ufadhili wa masomo kwa wakimbizi, Einstein German Academic Refugee Initiative (DAFI). Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).

Maadhimisho hayo yaliyofanywa na UNHCR Kwa kushirikiana na Kamati ya Kimataifa ya Uokoaji (IRC), yalifanyika jijini Dar es Salaam, tarehe 6 Desemba 2022, na kuhudhuriwa na baadhi ya viongozi wa kiserikali na mabalozi.

Akizungumza katika maadhimisho hayo Afisa Elimi wa UNHCR nchini Tanzania, Yank Yankeu, alisema ufadhili wa DAFI ni fursa pekee kwa wakimbizi wanafunzi kufanikisha masomo Yao,” alisema Yank.

Naye Naibu Mwakilishi wa UNHCR, George Kuchio, alisema kitendo cha kuwapa elimu wakimbizi kinachangia kutatua matatizo yaliyosababisha wakimbie nyumbani kwao.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa Jana tarehe 7 Desemba 2022 na UNHCR, mradi was DAFI ulioanzishwa 1992, umenufaisha wakimbizi 22,500 kutoka mataifa 55 ikiwemo Tanzania.

Kwa upande wa Tanzania, wakimbizi 460 wamenufaika na ufadhili huo tangu uanze 1992, ambapo wahusika walipata masomo yao katika Chuo Kikuu Cha Iringa, Chuo Cha Muhimbili, Chuo Kikuu cha Dodoma na Taasisi ya Usimamizi was Fedha (IFM).

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Kapinga kuongoza usambazaji wa mitungi ya gesi 10,000 ya Taifa Gas

Spread the loveNaibu Waziri wa Nishati, Judith Kapinga ameahidi kuongoza kwa ufanisi...

BiasharaHabari Mchanganyiko

Wafanyabiashara, wawekezaji China waridhia kuwekeza bil. 800 katika sekta 5 nchini

Spread the loveUJUMBE wa wafanyabiashara na wawekezaji wakubwa kutoka Jimbo la Changzhou...

Habari Mchanganyiko

Bil. 4.42 kumaliza uhaba maji kata 2 Musoma Vijijini

Spread the loveWANANCHI wa kata za Busambara na Kiriba, Jimbo la Musoma...

BiasharaHabari Mchanganyiko

Soko nepi za watoto lashuka, watu wazima lapaa

Spread the loveKiwanda cha kutengeneza nepi cha Japan kimetangaza kuwa kitaacha kutengeneza...

error: Content is protected !!