Monday , 6 May 2024
Home Habari Mchanganyiko Serikali yasaini mkataba kuongeza mapato gesi na mafuta
Habari Mchanganyiko

Serikali yasaini mkataba kuongeza mapato gesi na mafuta

Spread the love

SERIKALI kupitia Shirika la Mafuta Tanzania (TPDC), imesaini mkataba wa uzalishaji na ugawaji mapato (PSA) kitalu cha Ruvuma-Mtwara utakaoiwezesha kupata zaidi mapato. Anaripoti Mwandishi Wetu … (endelea).

Waliokaa kuanzia kushoto Meneja Mkuu wa kamapuni ya ARA Petrolium, Erhan Saygi; Waziri wa Nishati, January Makamba; Mkurugenzi Mtendaji TPDC, Dk. James Mataragio na Mkurugenzi Ndovu Resources, Charles Santos wakisaini mkataba huo.

Mkataba huo uliosainiwa leo tarehe 25 Novemba, 2022 umehusisha Wizara ya Nishati, TPDC na Kampuni za ARA Petroleum na Ndovu Resources na utaongeza mapato ya Serikali kutoka asilimia 68 hadi asilimia 75 ya mapato ghafi.

Akizungumza mara baada ya kutia saini mkataba huo Waziri wa Nishati, Januari Makamba amesema Tanzania imeandika historia kubwa baada ya miaka 12.

“Siku hii ni kubwa na ya kihistoria kwasababu Serikali inaenda kupata asilimia 75 ya mapato ghafi. Hii ndo tafsiri ya win-win na kazi hii imefanywa ndani yam waka mmoja,” amesema Makamba.

Makamba amesema Tanzania inaanza kuingia kwenye uchumi wa gesi, “si kwa tukio hili la leo tu lakini kwa mlolongo wa matukio na jitihada  za Serikali.”

Amesema wapo kwenye hatua ya mwisho wa majadiliano ya mradi wa kuchakata gesi mkoani Lindi utakaogharimu Sh 70 trilioni.

“Huu utakuwa uwekezaji mkubwa barani Afrika,” amesema na kuongeza kuwa “mpaka sasa visima viwili vimechorongwa katika kitalu hiki na kugundua gesi asilia kiasi cha futi za ujazo bilioni 466.

Amesema tafiti zinazoendelea zinaonyesha kitalu hiki kina jumla ya kiasi cha gesi cha futi za ujazo bilioni 1,642 hivyo kusainiwa kwa mkataba huu wa nyongeza ni hatua kubwa katika maandalizi ya kuendeleza gesi iliyogunduliwa na hivyo kuongeza uzalishaji wa gesi asilia nchini.

“Katika Mradi huu tunakadiria kuwekeza takribani dola za kimarekani milioni 500 katika kuendeleza gesi iliyogunduliwa. Katika uendelezaji na uzalishaji wa Kitalu cha Ruvuma, TPDC inatarajiwa kushiriki kwa 15%.

“Utekelezaji wa mradi huu unatarajia kuzalisha ajira kwa watanzania pamoja na kukuza uchumi wa nchi yetu kutokana na kodi na tozo mbalimbali zitakazopatikana kutokana mauzo ya gesi.

“Faida nyingine zitakazopatikana ni pamoja na matumizi ya gesi katika kuzalisha umeme ambayo kwa sasa gesi asili inachangia zaidi ya asilimia 60 kwenye gridi ya taifa, hivyo utekelezaji wa mradi huu utaongeza kiasi cha umeme unaozalishwa kutokana na gesi asilia, kuendesha viwanda, kutumia majumbani pamoja na kwenye magari,” amesema.

UJENZI CHUO CHA MAFUTA NA GESI WAIVA

Makamba na kuongeza kuwa Serikali imeamua kujenga Chuo cha politekniki mahususi kwa mambo ya mafuta na gesi.

“Ndugu zangu wa Lindi na Mtwara – sasa nchi yetu inaanza kuingia kwenye uchumi wa gesi. Sio kwa tukio hili la leo tu, lakini kwa mlolongo wa matukio mengine kutokana na jitihada za Serikali.

“Kule Arusha, tupo kwenye hatua za mwisho za majadiliano kwenye ule mradi wetu wa kuchakata gesi utakaogharimu zaidi ya trilioni 70. Huu utakuwa uwekezaji mkubwa barani Afrika,” amesema Makamba.

Pia amesema eneo la Lindi, serikali imeamua kujenga Chuo (Polytechnic) cha mambo ya Mafuta, Gesi na Umeme, ili kujengea uwezo  wananchi wa mkoa huo na watananzania kwa ujumla,” amesema.

“Lakini pia tutajenga ukanda maalumu wa uwekezaji (Special Economic Zone) ndani ya eneo la mradi ili kuchochea maendeleo ya Lindi na Mtwara baada ya mradi kukamilika,” amesema Makamba.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

AfyaHabari Mchanganyiko

Huduma za kibingwa zazinduliwa katika hospitali za halmashauri 184

Spread the loveSERIKALI imezindua huduma za matibabu za kibingwa katika hospitali 184...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Wizara ya Uchukuzi yaomba kuongezewa bajeti na Bunge

Spread the loveWIZARA ya Uchukuzi imeliomba Bunge liidhinishe bajeti yake kwa mwaka...

Habari Mchanganyiko

Prof. Mbarawa aanika mafanikio ya TMA

Spread the loveSHUGHULI za Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA), zimeimarika...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Serikali kutafuta mwekezaji mwingine Bandari ya Dar es Salaam

Spread the loveSERIKALI inaendelea kutafuta mwekezaji mwingine atakayeendesha gati namba nane hadi...

error: Content is protected !!