Sunday , 29 January 2023
Home Gazeti Habari za Siasa Uchaguzi huru na haki ni msingi wa demokrasia: Dk. Jingu
Habari za SiasaTangulizi

Uchaguzi huru na haki ni msingi wa demokrasia: Dk. Jingu

Spread the love

 

KATIBU Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge na Uratibu, Dk. John Jingu, amefunga warsha ya siku nne kwa makamishna na maafisa waandamizi wapya wa Tume za Uchaguzi ukanda wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika ECF-SADC, na kuwataka maafisa hao kwenda kutekeleza kwa vitendo yale waliojifunza ili kuwa na Uchaguzi huru na haki kwenye nchi zao. Anaripoti Jonas Mushi, Dar es Salaam … (endelea).

Dk. Jingu amefunga mafunzo hayo yaliyohusishawajumbe 60 kutoka nchi 9 wanachama wa ECF-SADC, leo Ijumaa tarehe 25 Novemba, 2022, jijini Dar es Salaam.

Amesema Uchaguzi ulio huru na wa haki na chanzo cha usalama na amani ya nchi na pia ni miongoni mwa nguzo zinazoashirika kuimarika kwa demokrasia katika nchi husika.

“Kupitia warsha hii washiriki ambao ni makamishna wapya, wakuu wa taasisi na maafisa waandamizi wamekumbushwa majukumu yao na wamejengewa uwezo utakaowasaidia kuhakikisha chaguzi katika nchi zao zinaendelea kuwa huru, za haki na zenye kuaminika,” amesema Dk. Jingu.

Amesema anamini baada ya mafunzo hayo hakutakuwa na chaguzi zenye changamoto ikizingatiwa kuwa nyingi zimejadiliwa katika warsha hiyo na kuona namna ya kuzitatua.

Amesema katika ukuaji wa teknolojia kuwekuwa na fursa na changamoto katika chaguzi ambapo amesema fursa zilizopo zitumike huku changamoto zikktafutiwa ufumbuzi.

Ameongeza kuwa kwa upande wa Tanzania imekuwa na jitihada za kipekee za kuhakikisha changamoto za uchaguzi zinapunguzwa ikiwemo kuzingatia mahitaji wa watu wenye uhitaji maalumu.

“Tunaporudi kwenye nchi zetu kutekeleza majukumu yetu ya kuongoza vyombo vya uchaguzi lazima tujue tunawajibu wa kuboresha chaguzi zetu na kuongeza uwezo katika kusimaia chaguzi. Tunapaswa kujiwekea malengo ya kuimarisha demokrasia katika ukanda wetu,” amesema Dk. Jingu.

Nchi tisa zilizoshiriki mafunzo hayo yaliyoanza tarehe 22, Novemba, 2022, ni pamoja na Tanzania, Zimbabwe, Namibia, Malawi, Eswatini, Lesotho, Ushelisheli, Botswana na Zambia.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoTangulizi

Haya hapa matokeo ya mtihani kidato cha nne 2022

Spread the loveBARAZA la Mitihani la Tanzania (Necta) leo Jumapili limetangaza matokeo...

Habari za Siasa

NCCR-mageuzi yawaangukia Polisi kupotea kwa kada wake

Spread the loveJESHI la Polisi nchini limeombwa kufanya uchunguzi wa kina utakaosaidia...

HabariTangulizi

Bakwata wamkangaa Sheikh wa Dar es Salaam

Spread the love  BARAZA la Ulamaa, limefutilia mbali uamuzi wa “kuvunja ndoa,”...

Habari za Siasa

Uamuzi kesi ya kupinga Bodi ya Wadhamini NCCR-Mageuzi kutolewa Februari 6

Spread the love  MAHAKAMA Kuu, Masjala Kuu ya Dar es Salaam, imepanga...

error: Content is protected !!