Thursday , 25 April 2024
Home Habari Mchanganyiko Mwandishi wa Raia Mwema ashinda tuzo COSTECH
Habari Mchanganyiko

Mwandishi wa Raia Mwema ashinda tuzo COSTECH

Spread the love

MWANDISHI Mwandamizi wa Gazeti la Raia Mwema, Selemani Msuya amekomba tuzo za mwandishi bora wa mwaka 2022 zilizotolewa na Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH). Anaripoti Mwandishi Wetu… (endelea).

Msuya ametwaa tuzo mbili ambapo ya kwanza ni Tuzo ya Mwandishi Bora wa Makala za Bioteknolojia na Tuzo ya ya Mshindi wa Jumla.

Msuya ametwaa tuzo hizo baada ya kuandika makala mbalimbali zinazohusiana na masuala ya bioteknolojia na uhandisi jeni ambapo alishiriki na waandishi wa vyombo vingine vya habari na kuibuka mshindi wa jumla.

Mwandishi Lucy Ngowi wa Gazeti la Habari Leo, ametwaa Tuzo ya Habari za Sayansi kwa Lugha  ya Kiswahili na Tuzo ya Mwandishi wa Habari za Sayansi wa wakati wote.

Naibu Waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia Omar Kipanga katika akiwa nna Mkurugenzi Mkuu wa COSTECH, Dk Amos Nungu kushoto wakati wa utoaji wa tuzo za uandishi wa habari za sayansi na bioteknolojia, kushoto kwa Dkt Nungu ni Mwandishi Mwandamizi wa Gazeti la Raia Mwema Selemani Msuya aliyeibuka mshindi wa jumla mwaka 2022, kulia kwa Waziri Kipanga ni Mwandishi wa Azam Tv Benson Eustace mshindi wa kipengele cha Tv na Lucy Ngowi mshindi wa Habari za Sayansi za Kiswahili.

Naye Mwandishi Benson Eustace wa Azam TV amekuwa mshindi wa Bora wa Vipindi vya Sayansi baada ya kuandaa vipindi mbalimbali.

Msuya na Benson pamoja na kushinda tuzo hizo katika ngazi ya nchi wamechaguliwa kushiriki shindano la mwandishi bora wa habari za bioteknolojia na sayansi Afrika ambazo zinafanyika jijini Abuja nchini Nigeria Desemba 2,2022.

Akizungumza baada ya kutoa tuzo hizo, Mkurugenzi Mkuu wa COSTECH, Dk. Amos Nungu alisema wametoa tuzo na zawadi kwa waandishi wanaondika habari za sayansi, ubunifu na bioteknolojia ili kuchochea uandishi wa habari unaogusa jamii.

Amesema pia COSTECH kwa kushirikiana na wadau wengine imekuwa ikitoa tuzo mbalimbali kwa vijana wabunifu wa teknolojia mbalimbali, hali ambayo inaongeza kasi ya ubunifu nchini.

“Tumetoa tuzo za vyeti na zawadi kidogo kwa waandishi wa habari watatu ambao wameandika habari za sayansi, ubunifu na bioteknolojia. Tunawasihi waandishi kuandika habari hizi kila mwaka tutaendelea kuwatambua,” amesema.

Naye Naibu Waziri Kipanga amesema Serikali itaendelea kuwezesha na kusaidia vijana wabunifu katika eneo lolote ambalo litaweza kuleta tija kwenye kuchochea maendeleo ya nchi.

Amesema katika kipindi hiki Serikali pamoja na wadau mbalimbali wametoa zaidi ya Sh.bilioni 1.1 kwa vijana wabunifu, waweze kuendeleza bunifu zao.

“Katika bajeti ya 2022/2023 Serikali ilitenga Sh.milioni 700, lakini wadau wa maendeleo kama SIDA wametoa zaidi ya Sh.milioni 450 katika eneo hilo la ubunifu,” amesema.

Amesema lengo la Serikali ni kuhakikisha bunifu ambazo zinabuniwa zinaenda sokoni kutatua changamoto ambazo zinakabili jamii.

Naibu Waziri Kipanga alitoa wito kwa wadau wa maendeleo wakiwemo Benki ya CRDB, NMB, Ufunguo na wengine kujitokeza ili kuwezesha wabunifu ambao wamekuwa wakibuni teknolojia zinazoenda kutatua changamoto za jamii.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

Exim Bank yatoa  vitanda kwa shule ya Jeshi la Polisi Moshi

Spread the love  BENKI ya Exim imekabidhii  seti ya vitanda kwa Shule...

Habari Mchanganyiko

NBC yakabidhi vitanda Shule ya Polisi Moshi

Spread the loveBenki ya NBC imekabidhi msaada wa vitanda 28 kwa Shule...

Habari Mchanganyiko

THRDC yaongeza mkataba wa ushirikiano na ABA

Spread the love  MTANDAO wa Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania (THRDC),...

Habari Mchanganyiko

Rufaa ya Equity Benki, State Oil yakwama

Spread the loveMAHAKAMA ya Rufani, jijini Dar es Salaam, imeshindwa kuendelea na...

error: Content is protected !!