Tuesday , 7 May 2024
Home Habari Mchanganyiko Tanzania, DRC zakubaliana kuboresha miundombinu
Habari Mchanganyiko

Tanzania, DRC zakubaliana kuboresha miundombinu

Spread the love

SERIKALI za Tanzania na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo DRC kwa pamoja zimeingia makubaliano ya  kuboresha miundombinu ya barabara, reli na bandari ili kuongeza ufanisi katika biashara na hivyo kukuza uchumi wa nchi hizo. Anaripoti Mwandishi Wetu … (endelea).

Hafla ya makubaliano hayo imefanyika jijini Dar es Salaam jana tarehe 9 Novemba, 2022 ambapo Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi wa Tanzania, Prof. Makame Mbarawa amesema makubaliano yataimarisha miundombinu ya reli, barabara, bandari na ujenzi wa meli za mizigo na abiria.

“Tunakusudia kuongeza ufanisi wa kibiashara katika nchi zetu na hivyo kuimarisha uhusiano wa kindugu na kukuza uchumi wa nchi zetu”, amesisitiza Prof. Mbarawa.

Prof. Mbarawa amesema miradi hiyo ambayo ujenzi wake utatekelezwa kwa awamu utapunguza muda wa safari kutoka DSM kwenda Lubumbashi nchini DRC na hivyo kupunguza gharama za biashara na muda wa kusafirisha mizigo toka siku 30 hadi wiki moja.

Waziri wa Miundombinu wa DRC, Alexis Mavunyi amesema namna mataifa hayo mawili yatakavyo nufaika kutachochea uzalishaji wa bidhaa, mazao na biashara zingine hivyo kukuza uchumi wa nchi hizo na raia wao.

Kwa upande wake, Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya Ushoroba wa Kati, Wakili Froly Okanju amesema  makubaliano hayo yatafungua fursa kubwa ya usafirishaji kwa nchi za ushoroba wa kati ambazo zinakwenda kupata maendeleo kwa kuwa zinaitegemea Tanzania katika uingizaji wa mizigo na hivyo kuitaka Tanzania kujipanga kuhudumia nchi za ushoroba huo kikamilifu.

Pamoja na mambo mengine ujenzi wa Miradi hiyo inayotarajiwa kuanza utekelezaji wake baadae mwakani itatoa fursa kwa Serikali za Tanzania, DRC, Wadau wa Maendeleo ya kuzalisha nafasi za ajira.

Viongozi hao pamoja na ujumbe wao wametembelea Shirika la Reli TRC na Mamlaka ya Bandari nchini TPA na kufurahishwa na namna taasisi hizo zinavyofanya kazi kwa weledi na ubunifu.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

BiasharaHabari Mchanganyiko

NBC, SILABU waungana kufikisha elimu ya fedha majumbani

Spread the loveBenki ya Taifa ya Biashara (NBC) imeingia makubaliano ya ushirikiano...

AfyaHabari MchanganyikoMakala & Uchambuzi

Kisukari cha mimba ni nini?

Spread the loveKisukari cha mimba ni aina ya kisukari kinachotokea kwa baadhi...

Habari Mchanganyiko

Mafunzo kwa bodaboda 395 yamkuna Meya Dodoma

Spread the loveNAIBU Meya wa Jiji la Dodoma, Asma Karama amepongeza mafunzo...

Habari Mchanganyiko

Samia aagiza huduma za dharura maeneo yaliyoathiriwa na kimbunga Hidaya

Spread the love   RAIS wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania, Samia...

error: Content is protected !!