Tuesday , 7 May 2024
Home Kitengo Michezo Serikali yaja na mfuko wa kukopesha wasanii bila riba
Michezo

Serikali yaja na mfuko wa kukopesha wasanii bila riba

Spread the love

 

Serikali inatarajia kuanzisha mfuko maalum kwa ajili ya kuwezesha wasanii wote nchini kupata fursa ya kukopa bila riba na kujikwamua kiuchumi pamoja na kukuza sanaa zao. Anaripoti Faki Sosi, Dar es Salaam … (endelea).

Hayo yamesemwa juzi tarehe 15 Oktaba 2022 na Mkurugenzi wa Maendeleo ya Sanaa Dk. Emanuel Ishongoma katika uzinduzi wa vazi la Tribe Called Afrika linaloitambulisha Tanzania na Afrika Dunia lililobuniwa na Mwanamitindo wa Kitanzania Dominic Godfrey.

Dk. Ishengoma alisisitia wasanii hao watakopa bila riba ili waweze kurejesha mikopo na wengine wapate fursa ya kukopa.

Aidha, akizungumzia vazi hilo alisema Serikali itahakikisha kuwa wasanii wanatimiza ndoto zao kimaisha na kuitangaza nchi kimataifa kupitia ubunifu wa mavai.

Katika kulitangaza vazi hilo, Mwanamitindo huyo ameshirikiana na Mwanamitindo na Msanii wa filamu kutoka nchini Uingereza, Oris Erhuero.

Alisema sekta ya ubunifu wa mavazi ni sekta ya kipekee ambayo inazidi kuitangaza nchi kimataifa.

Naye Katibu Mkuu wa Baraza la Sanaa (Basata), Dk. Kedmon Mapana alisifu vazi la ubunifu liliobuniwa na Godfrey na kusema kuwa vazi hilo ni kiashiria cha kuwaleta pamoja wafrika.

Alisema Serikali inamuunga mkono mbunifu huyo kwa jitihada zake ili kuhakikisha ndoto yake na vijana wengine inatimia

Dominic alisema vazi hilo ni ubunifu linaloonyesha uhalisia wa Mtanzania na Mwafrika.

“Nimetengeneza vazi hili kwa mkono kwa ushirikiano wangu na muigizaji kutoka Uingereza Oris,” alisema.

Alisema kuwa lengo la vazi hilo ni kuzidi kuitangaza Tanzania kwa kuwa linaonyesha uhalisia wa Watanzania.

Pia alishirikiana na Msanii Oris Kutembea kutembelea maeneo mbalimbali nchini na kupiga picha na vazi hilo kwa lengo la kuvitangaza vivutio hivyo.

Aidha, Msanii na Mwanamitindo maarufu nchini Uingereza,
Oris Erhuero alisema amefika nchi kwa ajili ya kumuunga mkono Dominic hasa ikizingatiwa vazi hilo litaitangaza Tanzania.

“Nimevutiwa na Tanzania ina sehemu nyingi nzuri tumekwenda Ngorongoro, Serengeti, Kilimanjaro na Zanzibar” alisema Oris.

Wakati Maria Charles mdau wa mitindo nchini alisema kuwa vazi hilo litakwenda kuiinua Tanzania kwenye daraja la kimataifa.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Michezo

Idris Sultan anogesha msimu wa 3 wa Bridgerton

Spread the loveSTAA wa burudani kutoka ardhi ya Tanzania, Idris Sultan amenogesha...

Michezo

Ligi mbalimbali za pesa kuendelea leo

Spread the love JUMAPILI ya leo imekaa kipesa tuu yani baada ya...

Michezo

Usiishie kuangalia tu game za leo, piga na mkwanja na Meridianbet

Spread the love  LIGI mbalimbali barani ulaya zitarejea tena Jumamosi ya leo...

Michezo

Ligi mbalimbali za pesa kuendelea leo

Spread the love Ijumaa ya leo ambapo mechi mbalimbali zinaendelea Duniani Meridianbet...

error: Content is protected !!