MSHAMBULIAJI hatari raia wa Ufaransa, Karim Benzema anayekipiga katika Klabu ya Real Madrid ya nchini Uhispania, ametwaa tuzo ya mchezaji soka bora wa dunia kwa mwaka 2022 ‘Ballon d’Or. Anaripoti Mwandishi Wetu… (endelea).
Benzema mwenye umri wa miaka 34, amemaliza tambo za nyota wawili wa mchezo huo duniani, Lionel Messi raia wa Argentina anayekipiga PSG ya Ufaransa na Cristiano Ronaldo raia wa Ureno anayesukuma gozi kwa Mashetani wekundu Manchester United.
Messi amechukua tuzo hiyo mara saba kwa nyakati tofauti na mara ya mwisho ilikuwa mwaka jana huku Ronaldo akibeba tuzo hiyo mara tano.
Licha ya Benzema kuingia katika kinyang’anyiro cha tuzo hiyo mara kadhaa, mwaka huu nyota imemuwakia huku umri wake kisoka ukiwa unalekea ukingoni.
Ili kuipata heshima hiyo, mwaka huu Benzema amewapiga vikumbo wachezaji bora kama Sadio Manne, Kelvin De Bruyne na Robert Lewandowski ambao ndio waliounda nne bora kabla ya kumpata mshindi.
Ushindi huo umekuja kutokana na mafanikio makubwa iliyopata klabu hiyo ya Real Madrid ambapo kwa msimu uliopita licha ya kuwa klabu bora ya dunia, pia Benzema aliisaidia timu hiyo kishinda taji la 14 la ligi ya Mabingwa Ulaya ‘Uefa Champions’.
Pia katika msimu uliopita Benzema aliisaidia klabu hiyo kushinda taji la 35 la ligi kuu ya Hispania maarufu kama La liga.
Hayo yanajiri wakati Ronaldo na Messi wakihaha kurejesha makali ya timu zao Manchester United na PSG.
Leave a comment