Friday , 3 May 2024
Home Kitengo Habari Kimataifa Mwanaye Museveni awapiga mkwara wapinzani, ‘nitawashinda baba akistaafu’
Kimataifa

Mwanaye Museveni awapiga mkwara wapinzani, ‘nitawashinda baba akistaafu’

Mtoto wa Rais wa Uganda, Yoweri Museveni, Muhoozi Kainerugaba
Spread the love

 

MTOTO wa Rais wa Uganda, Yoweri Museveni, Muhoozi Kainerugaba amezua mjadala mpya nchini Uganda kwa kudai kuwa ndiye rais anayefuata wa nchi hiyo. Inaripoti Mitandao ya Kimataifa … (endelea).

Muhoozi alionyesha imani kuwa upinzani chini ya mwanamuziki aliyegeukia siasa Robert Kyagulanyi ‘Bobi Wine’ hautafua dafu kuongoza nchi baada ya kustaafu kwa baba yake.

“Kwa upinzani wa Uganda, baada ya baba yangu, nitawashinda vibaya katika uchaguzi wowote. Waganda wananipenda zaidi kuliko watakavyowahi kuwapenda,” alisema kupitia Twitter tarehe 14 Oktoba, 2022.

Uganda inatarajiwa kufanya uchaguzi mkuu mwaka wa 2026 kumchagua rais mpya. Museveni ameiongoza nchi hiyo tangu alipoingia madarakani mwaka 1978.

Aidha, Bobi Wine ambaye ni kiongozi wa chama cha upinzani cha National Unity Platform, alitangaza azma yake ya urais kwa mara ya kwanza mwaka wa 2019 lakini akashindwa na Museveni katika uchaguzi wa 2021.

Hii si mara ya kwanza kwa Muhoozi kutoa maoni kuhusu mrithi wa urais kwani Mei 2019, Muhoozi alichapisha ‘meme’ inayoonyesha jinsi yeye na ‘kaka yake’ walivyokuwa waking’ang’ania nafasi hiyo.

Aliandika, “Mimi na kaka yangu mdogo Kabobi tukibishana kuhusu nani anaweza kujaza viatu vya baba yangu! Shukrani kwa msanii bora nchini Uganda.”

Akijibu tweet hiyo Bobi Wine alisema mimi sio kaka yako na wala sishindani na viatu vya baba yako, unastahili viatu vya M7, ng’ombe wake na hata kofia yake, kosa moja unalofanya ni kudhani Uganda ndio moja ya mali za baba yako ili urithi.”

Kiongozi huyo wa upinzani siku za nyuma alidai kuwa Museveni alikuwa akimtayarisha Muhoozi kuwania kiti hicho.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaKimataifa

Mwanamke Rwanda ataka kupambana tena na Kagame

Spread the loveKIONGOZI wa kihistoria wa upinzani nchini Rwanda, Victoire Ingabire Umuhoza,...

Habari MchanganyikoKimataifa

Ruto amteua Kahariri kuwa mkuu wa majeshi

Spread the loveRAIS wa Kenya, William Ruto, amemteua Jenerali Charles Muriu Kahariri,...

Habari za SiasaKimataifaTangulizi

Tanzania, Somalia kuibua maeneo mapya ya ushirikiano

Spread the love  RAIS Dk. Samia Suluhu Hassan, amesema Tanzania na Somalia...

KimataifaTangulizi

Mkuu wa majeshi Kenya afariki, Ruto atangaza maombolezo

Spread the loveRais wa Kenya, William Ruto ametangaza maombezo ya siku tatu...

error: Content is protected !!