NAIBU Waziri wa Madini Dk. Steven Kiruswa ameshiriki Mkutano wa pili wa Mawaziri wa Madini Afrika uliondaliwa na Umoja wa Afrika na kufanyika mjini Addis Ababa nchini Ethiopia. Anaripoti Mwandishi Wetu, Ethiopia … (endelea).
Mkutano huo umelenga kujadili mkakati wa pamoja wa nchi za Afrika kuhusu ugunduzi, uendelezaji na uvunaji madini hasusan vyanzo vya nishati safi yakiwemo madini ya Lithium, Nickel, Copper, Graphite, Manganese, cobalt, Vanadium ambayo ni muhimu kwa nishati ya magari ya umeme, umeme wa jua, batteries aina zote, transformer za umeme kwa lengo la kupunguza kiwango cha kaboni kwenye anga.
Maadini mengine ya kimkakati yaliyojadiliwa katika mkutano huo ni madini teknolojia ambayo ni REE, PGE, Phosphate, Niobium Tin.
Aidha, masuala yaliyojadiliwa ni pamoja na kuangalia Sera, Sheria na Kanuni zinazowezesha kuongeza manufaa kwa nchi za Afrika na wananchi wake kutilia mkazo suala la uongezaji thamani madini mkakati hadi zao la mwisho.
Vilevile, Serikali za nchi za Afrika zimehimizwa kujikita katika utafutaji madini badala ya kuziachia sekta binafsi haususan kampuni za kigeni pekee.
Mfano umetolewa kwa nchi ya Namibia ambayo Serikali yake kupitia Taasisi yake ya Jiolojia imefanikiwa kufanya utafiti wa madini nchi nzima ambapo hadi sasa pato kuu la Taifa hilo linategemea uchumi wa madini.
Mbali na hayo, mkutano huo umebainisha changamoto zinazozikabili nchi za Afrika katika sekta hiyo kuwa ni kutokana ni uwezo mdogo wa mitaji, uwezo mdogo wa kufanya tafiti za madini na teknolojia ndogo ya kuongeza thamani madini.
Mkutano huo umehudhuriwa na Mawaziri na Manaibu Waziri kutoka nchi za Tanzania, Zimbabwe, Zambia, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, Senegal, Sudani Kusini, Ethiopia, wawakilishi kutoka nchi za Namibia na Botswana pamoja na wadau wa sekta binafsi wanaojishughulisha na utunzaji wa mazingira na utafutaji madini.
Katika mkutano huo, Dk. Kiruswa aliongozana na Meneja wa Jiolojia kutoka Taasisi ya Jiolojia na Utafiti wa Madini Tanzania (GST), Maswi Solomon
Leave a comment