Saturday , 20 April 2024
Home Habari Mchanganyiko Mawaziri wa Madini Afrika wajadili ugunduzi, uvunaji madini mkakati
Habari MchanganyikoKimataifa

Mawaziri wa Madini Afrika wajadili ugunduzi, uvunaji madini mkakati

Spread the love

NAIBU Waziri wa Madini Dk. Steven Kiruswa ameshiriki Mkutano wa pili wa Mawaziri wa Madini Afrika uliondaliwa na Umoja wa Afrika na kufanyika mjini Addis Ababa nchini Ethiopia. Anaripoti Mwandishi Wetu, Ethiopia … (endelea). 

Mkutano huo umelenga kujadili mkakati wa pamoja wa nchi za Afrika kuhusu ugunduzi, uendelezaji na uvunaji madini hasusan vyanzo vya nishati safi  yakiwemo madini ya Lithium, Nickel, Copper, Graphite, Manganese, cobalt, Vanadium ambayo ni muhimu kwa nishati ya magari ya umeme, umeme wa jua, batteries aina zote, transformer za umeme kwa lengo la kupunguza kiwango cha kaboni kwenye anga.

Maadini mengine ya kimkakati  yaliyojadiliwa katika mkutano huo  ni madini teknolojia ambayo ni  REE, PGE, Phosphate, Niobium Tin.

Aidha, masuala yaliyojadiliwa ni pamoja na kuangalia Sera, Sheria na  Kanuni zinazowezesha kuongeza manufaa kwa nchi za Afrika na wananchi wake kutilia mkazo suala la uongezaji thamani madini mkakati hadi zao la mwisho.

Vilevile, Serikali za nchi za Afrika zimehimizwa kujikita katika utafutaji madini badala ya kuziachia sekta binafsi haususan kampuni za kigeni pekee.

Mfano umetolewa kwa nchi ya Namibia ambayo Serikali yake kupitia Taasisi yake ya Jiolojia  imefanikiwa kufanya utafiti wa  madini nchi nzima  ambapo  hadi sasa pato kuu la Taifa hilo linategemea uchumi wa madini.

Mbali na hayo, mkutano huo umebainisha changamoto zinazozikabili nchi za Afrika katika sekta hiyo  kuwa ni kutokana ni uwezo mdogo wa mitaji, uwezo mdogo wa kufanya tafiti za madini na teknolojia ndogo ya kuongeza thamani madini.

Mkutano huo umehudhuriwa  na Mawaziri na Manaibu Waziri kutoka nchi za Tanzania, Zimbabwe, Zambia, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, Senegal, Sudani Kusini, Ethiopia, wawakilishi kutoka nchi za Namibia na Botswana pamoja na  wadau wa sekta binafsi wanaojishughulisha na utunzaji wa mazingira na utafutaji madini.

Katika mkutano huo, Dk. Kiruswa aliongozana na Meneja wa Jiolojia kutoka Taasisi ya Jiolojia na Utafiti wa Madini Tanzania (GST), Maswi  Solomon

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

BiasharaHabari Mchanganyiko

Wauguzi, madaktari 1000 kugawiwa mitungi ya Oryx Gas

Spread the loveKAMPUNI ya Oryx Gas na Taasisi ya Doris Mollel Foundation...

Habari Mchanganyiko

Tanzania yachaguliwa Makamu wa Rais Tume ya Shirika la Hali ya Hewa Duniani

Spread the love  TANZANIA kupitia Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA)...

Habari Mchanganyiko

NEMC yaonya wanaojenga bila tathmini ya mazingira

Spread the loveBARAZA la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC),...

BiasharaHabari Mchanganyiko

NMB Pesa Akaunti yawavutia wakaguzi wa ndani Afrika

Spread the loveUbunifu wa bidhaa bora wa Benki ya NMB pamoja na...

error: Content is protected !!