November 30, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Bei ya mafuta yaendelea kushuka

Spread the love

BEI ya mafuta ya petroli imeendelea kushuka kwa miezi miwili mfululizo baada ya Mamlaka  ya Udhibiti wa Nishati na Maji kutangaza bei mpya za ukomo kwa mwezi Oktoba. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea)

Katika bei hizo ambazo zimeanza kutumika leo tarehe 5 Oktoba, 2022 katika mkoa wa Dar es Salaam lita moja ya petroli itauzwa kwa Sh 2,886, Dizeli Sh 3,083, mafuta ya taa Sh 3,275, ikilinganishwa na bei za mwezi uliopita za Sh 2969, Sh 3,125 na Sh 3,335 mtawalia.

Kwa mujibu wa taarifa ya EWURA iliyotolewa usiku wa kuamkia leo bei katika mkoa wa Tanga kwa lita moja ya petroli ni Sh 2,924, dizeli Sh 3,108 huku bei katika mkoa wa Mtwara petroli ikiwa ni Sh 2,908 na dizeli 3,099.

Mamlaka imewaagiza wafanyabiashara kuzingatia kuchukua mafuta katika bandari za karibu ambapo mikoa ya kaskazini inatakiwa kuchukua mafuta Tanga, mikoa ya kusini bandari ya Mtwara na mikoa ya kati bandari ya Dar es Salaam.

error: Content is protected !!