Friday , 3 May 2024
Home Habari Mchanganyiko Rais Samia ataka Sheria ya kulinda uwekezaji iangaliwe upya
Habari MchanganyikoTangulizi

Rais Samia ataka Sheria ya kulinda uwekezaji iangaliwe upya

Rais Samia Suluhu Hassan
Spread the love

RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ameonesha kutoridhika na masharti ya sheria ya kulinda uwekezaji inayoweka ulazima wa mzozo baina ya mwekezaji na Serikali kuamuliwa hapa nchini. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dodoma … (endelea).

Akizungumza katika Mkutano Mkuu wa Chama cha Mawakili wa Serikali uliofanyika leo Alhamisi tarehe 29 Septemba 2022 jijini Dodoma, Rais Samia amesema Sheria hiyo hailetoi picha nzuri kwa wawekezaji na badala yake inawafukuza na kumtaka Mwanasheria Mkuu wa Serikali kwenda kuitizama.

Mkuu huyo wa nchi amesema anayo mifano ya wawekezaji wanne waliokuwa tayari kuwekeza fedha nyingi kwa sharti la kutaka mizozo itatuliwe na mtu wa tatu lakini Serikali imeshindwa kwasababu ya uwepo wa Sheria hiyo.

“Nchi yetu inaingia mikataba mikubwa tu na nafahamu sheria zetu zinataka tunapopata mzozo na mwekezaji aanze au atumie Sheria zetu za ndani. Lakini kama mtu anakuja na fedha yake kubwa inaiwekeza ndani ya nchi tunakwenda na uwekezaji ule, mzozo unapotokea tunamwambia mimi nitakuhukumu, umekuja na fedha zako umekuja kuwekeza kwangu lakini ukitokea mzozo mimi nitakuhukumu nadhani haileti sura nzuri sana kwa wawekezaji na wengine wanatukimbia kwasababu hiyo,” amesema Rais Samia.

“Nina mifano hai mkononi kuna miradi mikubwa mitatu minne hivi , wawekezaji wamekuja na fedha nyingi sana, tumefanya mazungumzo tumefika katikati mwekezaji anasema unapotokea mgogoro twende kwa mtu wa tatu, usije kwangu, nisihukumiwe na wewe, twende kwa mtu wa tatu, sisi tukasema hapana mimi nitakuhukumu mwenyewe sasa wewe umekula pesa yake, amekupa ajira, uwekezaji upo kwako ukitokea mzozo unasema mimi nitakuhukumu tuwe wa kweli kuna haki hapo? amehoji Rais Samia.

“Pamoja na kwamba tunasema kwenye Sheria ya kulinda uwekezaji tuitizame vizuri, kuna mashauri kweli tunaweza kuyafanya hapa ndani lakini kuna ambayo mwekezaji ukimpa kipengele anakimbia. Niombe Ofisi ya Mwanasheria Mkuu ukaitazame hii nyie ndo wataalamu.”

1 Comment

  • Hongera kwa kuanzisha haya mazungumzo.
    Serikali za nchi zilizoendelea haziingii mikataba na makampuni binafsi ya nje. Bali wanawawezesha wazawa asilia halafu makampuni ya wazawa asilia yanaingia mikataba na makampuni ya nje.
    Pia watakiwe kuingia soko la hisa Dar baada ya miaka mitatu hata kama watajiuza kwa kampuni nyingine mpya.
    Nakutakia kazi njema.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Chadema waendelea kulilia katiba mpya

Spread the loveCHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimeendelea kudai upatikanaji wa...

Habari za SiasaTangulizi

Chadema kumshtaki Rais Samia

Spread the loveCHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimetishia kumfungulia kesi ya...

BiasharaHabari Mchanganyiko

NMB yang’ara maonesho OSHA

Spread the loveBenki ya NMB imebeba tuzo ya kampuni bora kwenye sekta...

Habari MchanganyikoKimataifa

Ruto amteua Kahariri kuwa mkuu wa majeshi

Spread the loveRAIS wa Kenya, William Ruto, amemteua Jenerali Charles Muriu Kahariri,...

error: Content is protected !!